Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba

WAKATI  tetesi na harakati za usajili zikiwa zinaendelea kushika kasi Bara Ulaya na kila pembe ya Dunia ,ikiwa ni kuzifanya klabu kuimarisha vikosi vyao kabla ya kuelekea kuanza kwa misimu , uwezo na ushirikiano aliouonesha nyota mpya wa Chelsea N'Golo Kante , pengine umeufanya klabu hiyo kujiweka kifua mbele na kuwa usajili wenye tija kunako klabu hiyo yenye makazi yake Stamford Bridge.

Hilo limejithibitisha katika mchezo wa kirafiki uliochezwa jana dhidi ya klabu ya soka ya AC Milan, ambapo Chelsea ilifanikiwa kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 3-1

Pengine klabu ya Chelsea ,unaweza kusema umempta mrithi  sahihi anayelingana uwezo na  aliyekuwa nyota wa zamani wa timu ya  Taifa ya Ufaransa na klabu ya Chelsea, Claude Makelele, lakini kiwango alichokionesha dhidi ya AC Milan akishirikiana na Nemanja Matic  hii inaonesha Chelsea wamesaini kiungo na nguzo ya msingi katika safu ya kiungo.

Kiungo huyo wa Timu ya Taifa ya Ufaransa, alianza mchezo huo na kutimiza majukumu yake akiwa mbele ya walinzi wa  Chelsea, huku akishirikiana vyema na viungo wenzake akiwemo, Nemanja Matic na Cesc Fabregas ambao walimsaisia kama viungo wa kati huku wakikamilisha mfumo wa 4-1-4-1. 

Kante , alifanikiwa kuingoza klabua ya soka ya Leicester City na kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza msimu wa 2015/16, huku akiwa ametengeneza ngome ngumu katika safu ya ulinzi na kuifanya klabu hiyo kuwa bora kutokana na kujiamni


(confidense)  kwake na kuongeza mafanikio ya klabu hiyo kabla ya kuanza kwa msimu.

Kwa maana hiyo, kuja kwa Kante, kutaifanya klabu hiyo kubadili mfumo (formation) wa uchezaji waliokuwa wakicheza msimu uliopita na kuifanya  klabu hiyo iwe na ulinzi zaidi kwa kutumia mfumo wa 4-1-4-1 kutoka 4-4-2 waliokuwa wakiutumia mwanzo.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline





Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.