Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba 

MENEJA mpya wa klabu ya Manchester United,Jose Mourinho , amesema kuwa ,Manchester United, itahitaji huduma angalau nyota mmoja ili kuimarisha kikosi chake na dili hilo litakamilika mapema na hayupo  kulizungumzia swalal lolote linalomuhusu  Paul Pogba.

Mourinho , amethibitisha kufanya usajili , ikiwa ni kipaumbele chake katika kuimarisha kikosi chake kabla ya msimu wa ligi kuu kuanza.

Kuhusu Pogba, klabu wameshafikkia pazuri juu ya uhamisho wa nyota huyo kutoka klabu ya Juventus kwa kiasi cha Paundi milioni 100 na kwamba nyota huyo anyemaliza mapumziko yake huko USA yupo kwenye maandalizi ya kupaa na kuja kujiunga na Manchester United.


United, walicheza mchezo wa kirafiki jana dhidi ya klabu ya Everton na kupelekea mchezo huo kumalizika kwa sare, huku tukishuhudia nahodha wa klabu hiyo, Wayne Rooney', akiukosa mchezo huo uliochezwa  kwenye Dimba la Old Trafford.
Baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Mourinho alikataa kuzungumzia chochote kinacho muhusu Pogba na kusema bado ni mchezaji halali wa klabu ya Juventus.
" Tunakwenda kufanya usajili wa mchezaji mmoja tu, huo ndio ukweli, lakini sitaki kuzungumzia kuhusu ,Paul Pogba, kwa sababu bado ni mchezaji wa  Juventus na pia sipendi kuona makocha wengine wakizungumzia wachezaji wangu napia sipendi kuzungumzia wachezaji wao". Alisema Mourinho
"Lakini usajili

wetu uliobaki ni wa mchezaji mmoja, mpaka dirisha la usajili litakapofungwa Augusti 31 tutapata muda wa kutosha wa nini tufanye, lakini nataka kufanya usajili huo kabla ya kuanza kwa msimu wa ligi kuu Uingereza" .Aliongeza Mourinho
Wakati Mourinho akiyasema hayo, United wanatarajia kukipiga dhidi ya klabu ya Leicer City kwenye mchezo wa ufunguzi wa ligi maarufu kama Ngao ya hisani 
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline






Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.