Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba

MKUU wa wailaya ya Ilala, Sophia Mjema, jana alifanya ziara ya ukaguzi wa kina wa magari ambayo yalipatiwa tenda ya kufanya usafi wa mazingira katika wilaya ya Ilala.


Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, akizungumza na wadau mbalimbali wa mazingira wakiwemo na waandishi wa habari jana  mara baada ya kuwasili katika viwanja vya Mnazi mmoja ambapo shughuli za ukaguzi wa kampuni zilizopewa tenda ya usafi na mazingira Wilaya ya Ilala zilifanyika

DC Mjema, amefanya ukaguzi huo wakatai wa kuelekea katika kuadhimisha siku ya mazingira Duniani ambapo kitaifa yanatarajiwa kufanyika mkoani Mara   huku kimkoa Wilaya ya Ilala ikipewa dhamana ya kuwa mwenyeji wa siku ya mazingira


Akizungumza na waandishi wa habari jana,katika viwanja vya Mnazi mmoja, DC Mjema,aliwataka wale wote ambao walipewa jukumu la kusafisha mazingira katika wilaya ya Ilala wahakikishe wanazingatia muda pia kuhakiksha ubora wa magari yao yapo salama kwa ajili ya kazi huku akisisitizia uwajibikaji imara wa kampuni hizo wakati wa kukusanya taka taka



"Kampuni amabazo mlipewa tenda ya usafi na mazingira kwanza mnatakiwa kuangalia ubora wa magari yenu kama yapo salama maana tunaweza kuwa na magari ya ukusanyaji taka ambapo pia ni taka,  hivyo hakikisheni mnatumia nyavu nzuri katika gari zenu kuhakikisha taka haianguki hovyo halikadahrika mtoe elimu kubwa kwa wale mnaowafuata wakati wa ukusanyaji taka wilaya yetu imepewa dhamana ya usafi kimkoa hivyo hatuna budi kutumia nafasi hiyo kuwakikishia hawajakosea kutupa dhamana ya kuwakilisha mkoa wa Dar es salaam "alisema  DC Mjema



Aidha, DC Mjema alisema kuwa, mkoa wa Dar es salaama unazalisha tani elfu sita kwa siku hivyo amaewataka wakandarasi wanaopewa tenda hizo watoe elimu kuhusu uzalishaji wa taka huku akifafanua kila taka ziwekwe katika makundi yake ili iwe rahisi katika ubebaji hivyo amewaomba kufanya kazi kwa bidii kuhakiisha wilaya ya Ilala inakuwa ya  kwanza katika mkoa na hata kitaifa.

Hata hivyo, Meneja wa uhusiano wa kampuni ya Gin Investment, Gerald Hall, alisema kuwa moja ya changamoto zinazowakabili ni pamoja na uelewa mdogo wa wananchi dhidi ya utupaji taka hovyo bila ya mpangilio wa sehemu husika, sehemu ya kuhifadhia taka kabla ya kupeleka dampo, uhaba wa madampo ya kuhifadhia taka hivyo aliiomba serikali kuangalia changamoto hizo huku akiwataka wawajibike katika kutoa elimu kwa viongozi wake kuanzia ngazi ya Kata, Wilaya  na hata Taifa kuhusu mazingira.


Miongoni mwa Makampuni yenye magari ambayo yalipatwa kukaguliwa na DC Mjema mara baada ya kupatiwa tenda ya kuweka mazingira safi katika Wilaya ya Ilala ni pamoja na Green Investment ltd, Tirima iliyopo Upanga mashariki na magharibi, Aifola, Kajenjere mchikichini, Pik iliyopo gerezani na Gin investment.




JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia website
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, 
insta@wabunifumediaonline

.
 


Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.