Na Yusuph Mwamba
MKUU mkoa wa Dar es salaam Mh: Paul Makonda, amefanya ziara ya kukagua mradi wa ujenzi wa Barabara za juu (Fly over ) katika eneo la Tazara Jijini Dar es salaam ikiwa ni pamoja na kuhoji pesa wanayopewa wafanyakazi wanaofanya kazi katika mradi huo.
Aidha, Mh: Makonda katika mahojiano na wakandarasi pamoja na wasimamizi wa mradi huo mara baada ya kukagua mradi, kwanza aliwapongeza kwa jitihada walizoonyesha tangia hatua ya awali hadi sasa ila aliwaeleza kuwa Serikali ya awamu ya tano inataka kila mradi unaosimamiwa ni lazima ukamilike haraka kwa mujibu wa muda waliopatiwa.
Aidha RC Makonda, aliitaka kampuni ya LABA inayoshughulika kuajiri vibarua kutoa maelezo kuhusu ujira na namna wanavyofanya mchakato wa kuwapata vibarua baada ya kulalamikiwa na vijana wanaofanya kazi katika mradi huo kuwa wanalipwa ujira mdogo na baadhi yao kusema kuwa kunapesa wanakatwa na kampuni hiyo baada ya kutafutiwa kazi.
“Naomba siku ya jumanne uniletee maelezo ofisini kwa ngu namna unavyo fanya katika kuwa pata na kuwalipa vijana hawa na wewe unalipwa bei gani kwanamna ulivyo nieleza hapa kumlipa mtu shilingi elf kumi kwa kazi hii ngumu sisawa hapo hapo katika hiyo hela atoe nauli pesa ya chai na chakula hapo sasa anabakiwa na nini ? ukileta tuta linganisha kamahaya malipo unayo walipa nisawana miradi migine ya kamaile ya TIB , magomeni .Kazi inayofanyika ni nzuri ila tunataka nao hawa vijana nao wafaidike na kazi wanayo fanya “ alisema Makonda.
Akizungumza na wafanyakzi vibarua amewapongeza kwa kufanya kazi kwa umakini kwa kuwa hadi sasa hakuna tukio la ajali iliyotokea hadi sasa ,na pia hakuna tukio la wizi lililo tokea kumekuwa na uadilifu na uamifu,na kuwa taka kufanya kazi kwa bidii.
“Nataka niwaambie hakuna njia ya short cut katika maisha wekeni malengo na kuweka akiba ilimsije mkawatu histori mlijenga daraja angalau na nyi mpite baadaye katika daraja hili, pia niwatake wananchi wa mkoa wa Dar es salaam tuitunze hii miundo mbinu kwa ajili ya vizazi vijavyo serikali ina tumi fedha nyingi sana kuijenga ‘’ alisema
Regnard Kaganga ni Mhandisi wa kampuni ya Oriontal Consutant Global amesema katika ujenzi huo huo umefikia hatua nzuri ya asilimia 40 na upande wa kasikazini wamesha anza kumwaga zege na upande kusini bado wanaendelea na kufunga majukwaa na kwamesha weka nguzo za daraja na kuahidi kuwa ujenzi utakamilika kwa wakati.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia website
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
.
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
.
Post a Comment