Halloween party ideas 2015
Image

 Na Mwandishi wetu, Dar es salaam

TANZANIA ni nchi inayo ongozwa kwa misingi ya demokrasia na katiba, nchi yoyote ili iweze kusimama lazima iwe na katiba yake na wanachi pamoja na viongozi waitambue na kuilinda.


                           Katiba ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania
                                          SURA YA KWANZA
      Hakika kupigia kura Sheria ya  1984 na.15.ibala.6 Sheria ya 2000 na.3ibara.4
5.(1) Kila raia wa Tanzania aliyetimiza umri wa  miaka kumi na minane     anayo haki ya kupiga kura
katika  Uchaguzi unaofanywa na wananchi. Na hakika  hii itatumiwa kwa kufuata masharti  ya
ibara ndogo  ya (2) Pamoja na masharti mengineyo ya katiba  hii na ni ya sheria  inayotumika nchini Tanzania kuhusu  mambo ya uchaguzi.


    (2) Bunge  laweza kutunga sheria na kuweka   masharti  yanayoweza  kuzuia  raia asitumie haki ya Kupiga kura  kutokana na yoyote kati ya sababu zifuatazo,yaani raia  huyo-
    a . Kuwa na uraia  wanchi nyingine:
    b.  Kuwa na ugonjwa  wa akili:
    c.  Kutiwa hatiani  kwa makosa Fulani ya jinai:
  d.   Kukosa au kushindwa kuthibitisha au kutoa kitambulisho cha umri,uraia au uandikishwaji  kama  mpiga kura,

      Mbali na sababu  hizo hakuna sababu nyingine yoyote inayoweza kumzuia  raia asitumie haki ya kupiga kura

(3) Bunge litatunga Sheria  ya Uchaguzi  na kuweka masharti  mambo yafuatayo-

(a)Kuanzisha Daftari la kudumu la wapiga kura,na kuweka utaratibu  wa kurekebisha  yaliyomo
Katika   Daftari hilo:

(b) kutaja sehemu na nyakati za kuandisha wapiga kura na kupiga kura:

(c) Utaratibu  wa kumwezesha mpiga kura   aliyejiandikisha  sehemu  moja kupiga kura Sehemu nyingine  na kutaja masharti ya utekelezaji wa utaratibu huo.

(d) Kutaja kazi na shughuli za Tume ya Uchaguzi na utaratibu wa kila uchaguzi ambao utaendeshwa chini ya uongozi na usimamizi wa Tume ya Uchaguzi.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline

  


Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.