SHIRIKA la Afya Duniani limeshauri matumiz ya Kondomu kwa
wapenzi ili kuepuka na hatari ya magonjwa ya zinaa kama kisonono,kaswende na
pangusa ambayo yamekuwa ni tishio Kubwa duniani kwa kizazi cha sasa.Magonjwa
hayo huwakumba mamilioni ya watu duniani kwasasa tofauti na zamani na kupelekea
hatari ya kukumbwa na magonjwa na watoto kuzaliwa walemavu.Kila mwaka huwakumba
watu wapatao milioni 131 kwa ugonjwa wa pangusa milioni 78 ugonjwa wa kaswende
na watu wapatao milioni 5.6 ugonjwa wa kisonono duniani kote.
Ugonjwa wa
kaswende husababishwa na bakteria ajulikanae kama Neisseria gonorrhoeae na
ugonjwa wa kisonono husababishwa na bakteria aina ya treponema palldum uku
ugonjwa wa pangusa ukisababishwa na bakteria aina ya Chlamydia trachomatis.
Mkurugenzi wa
shirika la afya duniani kitengo cha uzazi na utafiti Dk Lan Askew alisema kuwa
miongoni mwa hatua za kupunguza magonjwa matatu ya zinaa tajwa ni matumizi ya
kondomu kwa wapenzi na usahihi wa dawa kwa ugonjwa husika.Mkurugenzi uyo
aliagiza nchi zote duniani kufuata kanuni mpya za kuzuia magonjwa ya zinaa kwa
kutumia kondomu na kupendekeza kuwa kondomu ni miongoni mwa njia bora kuepuka na magonjwa ya zinaa.Magonjwa kama
kisonono,kaswende na pangusa yakiwa sugu mwilini bila kutibiwa husababisha
magonjwa ya kizazi kwa mwanamke ikiwapo kutoka kwa mimba na husababisha ugumba kwa
baadhi ya wanawake.Pia magonjwa haya matatu ya zinaa yasipotibiwa kwa wakati
hupelekea hatari ya kupata maambukizi ya Virusi Vya UKIMWI kwa haraka zaidi
kuliko asiekuwa na magonjwa ayo ya zinaa.
Mbali na
mkurugenzi huyo kupendekeza matumizi ya kondomu katika kuzuia maambukizi ya
magonjwa ya zinaa alielezea kuwa matumizi sahihi ya dawa kwa ajili ya magonjwa
ayo ya itumike dawa ya benzathine penicillin kwa ugonjwa wa kisonono na dawa ya quinolones kwa kwa
ajiri ya ugonjwa wa kaswende.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment