Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba
ELIMU kwa maana pana ni tendo au uzoefu wa athari ya kujenga akili, tabia ama uwezo wa kimaumbile wa mtu binafsi. Katika dhana ya kiufundi, elimu ni njia ambayo hutumiwa makusudi na jamii kupitisha maarifa, ujuzi, na maadili kutoka kwa kizazi kimoja hadi kingine.


Waalimu katika taasisi za elimu huratibisha elimu ya ia wao kupitia masomo kama vile ya kuandika, kusoma, hesabu au hisabati, sayansi  na historia. Mbinu hii wakati mwingine huitwa masomo haswa tunaporejelea somo la aina fulani kwa kawaida mbinu hii hutumiwa na maprofesa katika taasisi za masomo ya juu.


Chini ya mpango wa elimu kwa wote ulioanzishwa na Shirika la Elimu, sayansi na utamaduni la Umoja wa Mataifa ( UNESCO) nchi nyingi zimejitolea.


Nchini Marekani na Kanada, elimu ya msingi na sekondri kwa pamoja hurejelewa kama elimu ya K-12, na katika nchi ya New zeland, alimu hii hurejelewa kama elimu ya miaka 1-13. Azma ya elimu ya sekondari ni kutoa maarifa  ya kawaida, kutayarisha wanafunzi kwa elimu ya juu au kuwafunza watu kazi moja kwa moja.

Katika nchi yetu wengi wao hawajui kusoma na kuandika kitu ambacho kinapelekea kushuka kwa kiwango cha elimu hapa nchini.

Ripoti ya Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (Unesco) inasema watu wasiojua kusoma na kuandika Duniani wamefikia 774 milioni huku hali ikiendelea kuwa mbaya katika bara la afrika.
Ripoti hiyo inaeleza wazi kuwa idadi kubwa ya watu hao wasiojua kusoma na kuandika wengi wao wanaishi katika bara ya Afrika na Asia, na kwamba takwimu hizo zinaonyesha kiwango hicho kimeongezeka wa asilimia nane kuanzia mwaka 1990 hadi leo.

Ripoti hiyo inaeleza wazi kuwa idadi kubwa ya watu hao wasiojua kusoma na kuandika wengi wao wanaishi katika bara ya Afrika na Asia, na kwamba takwimu hizo zinaonyesha kiwango hicho kimeongezeka wa asilimia nane kuanzia mwaka 1990 hadi leo.
Kwa upande wa Tanzania hadi kufikia mwaka 2002 idadi ya watu wasiojua kusoma na kuandika ilikuwa watu 6.2 milioni. Idadi hiyo ni kwa watu wenye umri wa miaka 15 na kuendelea ambao ni sawa na asilimia 31, lakini kwa sasa idadi hiyo imeongezeka na kufikia watu zaidi ya milioni 14 hali ambayo ni ya hatari kwa maendeleo ya taifa.
Kwhiyo serikali inatakiwa kujikita zaidi katika kutatua changamoto hizi, ikiwemo kuboresha makazi ya waalimu, miaatala, mazingira rafiki juu ya wanfunzi pamoja na kuongeza nguvu yani kuhakikisha wizara husika ya Elimu na mafunzo ya ufundi inatengewa bajeti ya kutosha ili kufanikisha kukua na kuongezejka kwa elimu hapa nchini.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline



Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.