Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba

KUMEKUWA  utamaduni wa muda mrefu hapa nchini kuwa na mashindano ya walimbwende ma ‘Miss’ lakini warembo hao wamekuwa wakisikika kipindi cha mashindano tu na baada ya hapo tija yao huwa haionekani tena, lakini Mkuu wa wilaya ya Ilala Sophia Mjema amekuja na mbinu mpya  itakayo wawezesha washiriki wa mashindano hayo kuwa karibu na jamii na kuleta tija kwa Taifa letu. 
Akizungumza na waandishi wa habari kama mgeni rasmi katika mashindano ya Miss Ilala yaliyo fanyika jijini Dar es Salaam Kilimanjaro Hotel, Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema, amesema kuwa, wilaya yake ita hakikisha inawapa uhuru washiriki wote wa Miss Ilala, kuchagua jambo la kufanya na kulisimamia ili wawe mabalozi kwenye kata zao.

Aidha DC Mjema, alienda mbali zaidi huku akitolea mfano kuwa warembo hao wachague kuwa mabalozi wa Madawa ya Kulevya, Ndoa za Utotoni, Mazingira, Maadili ya Kinamama, Watoto na mengine yenye kufanana na hayo.




Na kuongeza kuwa wilaya yake itafanya kazi na washiriki hao wa Miss Ilala 2016 kwa mwaka mmoja kama mabalozi, ili wasikae mtaani bila ya kuwa na shughuli ya kufanya huku akiahidi kutoa ushirikiano wa dhati kwa kulisimamia suala hilo ipasavyo.


Mashindano hayo ya Miss Ilala yamehitimishwa kwa kumuibua Julitha Kabete kuwa mshindi kati ya washiriki 14 wa taji hilo  washiriki wengine ni Osmunda Mbeyela, Mercy Zephania, Melody Tryphone, Dalena David, Nuru Kondo, Sporah Luhende, Queen Nazil, Lilian Omolo, Mariam Maabad, Brenda Allan, Sabrina Halifa, Agriphina Nathaniel na Grace Malikita.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline




Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.