RYAN GIGGS ATUNDIKA DARUGA UNITED
Na Yusuph Mwamba
MKONGWE wa soka na aliyekuwa meneja msaidizi wa klabu ya Manchester United, Ryan Giggs amestaafu rasmi kuitumikia klabu Manchester United baada ya kuitumikia kwa miaka 29 tangu atue kunako klabu hiyo.
Giggs, alitua na kujiunga na klabu ya Manchester United mwaka 1987, miongoni mwa mafanikio aliyoyapata katika klabu hiyo ni pamoja na Kutwaa kombe la ligi mara 13, kombe la shirikisho la FA
mara 4, Ngao ya Hisani mara 8, huku akifanikiwa kutwaa makombe mawili kwa kila ligi kama Uefa super cup mara mbili, kombe la mataifa mara mbili,Champion League mara 2na kombe la dunia la vilabu mara mbili
Mchango wa Giggs ulikuwa mkubwa hadi kufikia uongozi wa klabu hiyo kumkabidhi kocha mchezaji baada ya kuondoka kwa aliyekuwa kocha wa klabu hiyo David Moyes na baadae kukabidhiwa kocha msaidizi chini ya aliyekuwa meneja wa klabu hiyo Lous Van Gaal aliyetimuliwa baada ya uongozi wa klabu ya United kutoridhishwa na mwenendo wa kocha huyo.
Kwa upande wa makamu mwenyekiti wa klabu ya Manchester United, Ed woodward, amesema kuondoka kwa Giggs kumewashtua wengi lakini akasisitiza washabiki wawe na amani kuwa wanaamini Giggs bado atakuwa na ushauri juu ya klabu hiyo licha ya kujiondoa katika nafasi yake ya kocha msaidizi.
"Giggs ni mchezaji mzuri, ni winga ambaye hajapatiwa mrithi wake kwanza anajituma sana uwanjani pia alikuwa ni mchezaji mwenye kipaji kikubwa cha kusoma mchezo dhidi ya wapinzani na amekuwa katika ushawishi wa kutengeneza hari ya ushindi wa klabu hakika tutamisi sana vitu vyake".Alisema Ed Woodward
Post a Comment