Halloween party ideas 2015
Image

PENATI YAIBEBA UJERUMANI "NUSU FAINALI EURO 2016

Na Yusuph Mwamba

MABINGWA wa kombe la Dunia mwaka 2014, timu ya Taifa ya Ujerumani ,imejikuta ikifanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya Euro 2016 kwa taabu, baada ya mchezo huo kuamuliwa kwa chanagamoto ya mikwaju ya penati dhidi ya timu ya Taifa ya Italia mchezo uliochezwa jana Jijini Ufaransa
Kocha wa timu ya Taifa y  Italia , Antonio Conte, akijaribu kutoa maelekezo kwa wachezaji wake jana kwenye mchezo wa kuwania kufuzu hatua ya nusu fainali Eoro 2016 dhidi ya timu ya Taifa ya Ujerumani
Benedikt Howedes, Thomas Muller na Mats Hummels wakisherekea ushindi wao walioupata jana dhidi ya Italia ,baada ya kufanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali Euro 2016


Mpaka mapumziko, timu hizo ziliweza kwenda vyumbani baada ya kutoshana nguvu ya bila kufungana 0-0
Stefano Storado akijaribu kuokoa hatari mbele ya Jonas Hector jana

Kipindi cha pili , timu zote zilionekana kushambuliana kwa kasi,kutokana na mchezo ulivyo na ubora wa timu zote mbili katika viwango vya soka Dunia, huku Ujerumani wakionekana kuutawala mchezo zaidi ya Italia.
Thomas Muller akijaribu kuwatoka walinzi wa timu ya Taifa ya Italia jana

Kunako dakiak ya 65 ya mchezo, mwanandinga wa Kimataifa na klabu ya Arsenal, Mesut Ozil, aliiandikia Ujerumani bao la kuongoza, kabla ya nyota , Leonardo Bonucci, kuisawazishia timu ya Italia bao kunako dakika ya 78 ya mchezo ya lala salama.
Ozil akishangilia goli lake la kwanza  dhidi ya timu ya Taifa ya Itali



Hadi kipyenga cha mwamuzi kinapigwa , timu hizo zilimaliza mchezo hu kwa kutoshana nguvu ya kufungana bao 1-1.
Leonardo Bonucci akishangilia bao lake baada ya kusawazishia Italia bao hilo kwenye mchezo wa jana hatua ya robo fainali Euro 2016



Licha ya kuongezwa kwa dakika, Lakini kila timu ilionekana kucheza kwa tahadhali kubwa  na hatimaye mchezo huo kuuamuliwa kwa changamoto ya mikwaju ya penati.
Kocha wa Ujerumani , Joachim Low akishangilia ushindi walioupata jana dhidi ya Italia

Hata hivyok, Ujerumani ilifanikiwa kuvuka hatua ya nusu fainali ya michuano ya fainali ya Euro 2016 kwa jumla ya changamoto ya mikwaju ya penati ya 6-5.

Kwa matokeo hayo , Timu ya Taifa ya Ujerumani inasubiri mshindi kati ya Ufaransa au timu ya Taifa ya Jamhuri ya Ice land katika hatu ya nusu fainali inayo tatarajia kupigwa Julai 7, 2016

Leo kuna mchezo mmoja unaowakutanisha wenyeji wa mashindano ya fainali ya michuano ya Euro 2016 timu ya Taifa ya Ufaransa dhidi ya timu ya Taifa ya Ice land.


Kikosi cha Ujerumani : Neuer, Hector, Howedes, Hummels, Khedira (Schweinsteiger, 16), Ozil, Muller, Boateng, Kroos, Kimmich, Gomez (Draxler, 72).
Kikosi cha Italia : Buffon, Florenzi (Darmian, 86), Barzagli, Bonucci, Chiellini (Zaza, 120), De Sciglio, Parolo, Sturaro, Giaccherini, Eder (Insigne, 108), Pelle.
Mchezaji bora wa mechi : Mats Hummels

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.