RALEIGH INTERNATIONAL" YAJA NA UKOMBOZI KWA VIJANA WA
KITANZANIA.
.Na Yusuph Mwamba.
Baadhi ya anashirikja wa kujitolea wa Raleigh Internatinal wakiwa katika moja ya harakati ya majukumu yao |
Rais wa Awamu ya Kwanza ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, amewahi kukaliliwa akisema kuwa Taifa lolote likitaka kuendelea lazima liwekeze kwa vijana kwani ndio nguvu kazi ya Taifa ambayo hupelekea kwenye chachu ya Maendeleo.
Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Kwanza wa Jamhuri wa Tanzania akizungumza juu ya uwajibikaji kwa Vijana |
Raleigh International, ni moja ya mashirika Duniani yanayo wakutanisha vijana wa nchini Tanzania na Uingereza ili kuleta mabadiliko kwa kufanya kazi kwa ukaribu na jamii ambapo huendesha miradi ya Ujasiriamali na Usafi wa Maji, Afya na Mazingira sehemu mbalimbali nchini ili kuongeza uelewa kwa wananchi na hii ni moja kusaidia ufanikishwaji wa Mpango wa Maendeleo Endelevu ya Dunia.
Baadhi ya wanashirika wa Raleigh ambao wamejitolea, wakiwajibika baada ya kukabidhi misaada kunako shule moja ijulikano kama shule ya msingi Nhungu Mkoani Njombe Wilaya ya Makete kata ya Nhungu |
Ahmed Mohamed Kilombo ni mmoja wa watanzania aliyepata nafasi ya kushiriki kwa kuungana na vijana kutoka Uingereza na kutoa elimu sehemu mbalimbali nchini Tanzania, ikiwemo Morogoro, Njombe na Iringa, huku ikiwa inakumbukwa shirikia hilo limefanya kazi takribani ya Miaka Mitatu katika kuleta mabadiliko katika dunia na kufanya panakuwa mahala salama pa kuishi.
Ahmed Mohamed Kilombo, akizungumza na baadhi ya wanafunzi wa TPSC juu ya mpango wa shirika la Raleigh |
Akitoa elimu ya mambo aliyojifunza Mbele ya Wanafunzi wa Chuo cha Utumishi wa Umma Magogoni (TPSC), yakiwemo Malengo ya kumi na saba ya Dunia (Sustainable Development Goals), huku akijikita kwenye matokeo chanya ya Malengo hayo ambapo ameeleza kuwa malengo hayo ni muhimu sana kuyajua kwani yanapelekea uwepo wa Afya stahiki, Mazirngira Safi haki sawa kwa mwanamke na mwanaume kwa ngazi ya jamii, na kwa Taifa kwa ujumla kuwa na Sera ambazo zitachagiza uwepo wa miundombinu endelevu yenye tija ya kutatua changamoto zilizopo kwenye Afya, Elimu, Uchumi, Jinsia na masuala yote mtambuka.
Click here to Reply or Forward
|
Post a Comment