|
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania , Dr John Pombe Magufuli |
Akizungumza jijini Dar es Salaam ,Mkurugenzi wa Baraza la Waganga na Watafiti wa Tiba Asili Halmashauri ya Wilaya ya kinondoni, Tabibu Maxmilian Lyana, ambapo ameeleza kuwa Serikali inatakiwa kuwa makini na makanjanja wa Tiba Asilia kwani wengi wao wamekuwa wakiwasababishia madhara makubwa watumiaji wa dawa hizo na kupelekea kuongezeka kwa wingi wa utapeli katika tasnia hiyo ya Utabibu.
‘’kuna waganga feki wengi sana ambao kazi yao ni kutapeli tu na hakuna tiba yoyote wanayoitoa na badala yake wanajikuta wakiwasababbishia madhara watumiaji wa Tiba hiyo". Alisema Lyana
|
Mkurugenzi wa Baraza la Waganga na Watafiti wa Tiba Asilia Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni, Maxmilian Lyana |
Aidha Tabibu Lyana ameongeza kuwa tasnia hiyo imefikia katika hali mbaya zaidi kiasi kwamba waganga wa tiba asili kuonekana kuwa ni kituko na heshima waliokuwa nayo imepotea na hawaaminiki tena kwa wateja wao kutokana na kuaribiwa jina na baadhi ya watu wachache ambapo ameishauri serikali kufuta vituo vyote vya waganaga wa tiba asili ambavyo havija sajiliwa na kuwataka wananchi kutokwenda kupata huduma kwa matapeli na kuwataka kutoa taarifa pale wanapotapeliwa na waganga feki.
|
Baadhi ya dawa za Asili zinazotumika kwa matibabu ya magonjwa mbalimbali |
|
Mtabibu mmoja akijaribu kutoa bei elekezi ya madawa hayo ya kitabibu |
Mtaalam huyo wa tiba asili wa kituo cha Ifakara Herbal Clinic, kilichopo Tandale sokoni, amesema kituo chake kinajishulisha na magonjwa mbalimbali ikiwemo matatizo ya uzazi, kisukali, Presha ya kupanda na kushuka,uvimbe,kifafa na kupooza huku akiiongeza kuwa hakuna uhusiano wowote kati ya waganga asili na mauaji yanayoendelea kutokea dhidi ya albino kwani tangu ameanza kufanya kazi hiyo hajawahi kuona kiungo cha mtu wenye Ualbino kinatumika kwa kupata utajiri na kuongeza kuwa mwenye kutaka utajiri afanye juhudi ili aweze kufanikiwa.
|
Maxmilian Lyana, Mkurugenzi wa Tiba Asilia Halmashauri ya Wilaya ya Kinondoni |
Post a Comment