Na Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
Taasisi
ya Moyo Jakaya Kikwete (JKCI) kwa kushirikiana na Taasisi ya Okoa Moyo
wa Mtoto (Save a Child’s Heart – SACH) ya nchini Israel zimewapeleka
watoto sita (6) wenye umri wa mwaka mmoja hadi miaka kumi na tatu
nchini Israel kwa ajili ya matibabu ya moyo.
Katika
safari yao ya matibabu nchini humo watoto, wauguzi pamoja na wazazi wao
wameondoka alfajiri ya jana tarehe 10/12/12. Baada ya matibabu ya
watoto kukamilika Maafisa Wauguzi wawili watabaki kwa ajili ya
kuhudhuria mafunzo ya mwaka mmoja ya jinsi ya kuwahudumia wagonjwa
waliopo katika wodi ya uangalizi maalum (ICU) na chumba cha upasuaji.
Taasisi
yetu inatibu magonjwa mbalimbali ya moyo kwa watoto kupitia wataalamu
wazalendo tulionao. Hata hivyo tunamkataba na Israel kwa baadhi ya
wagonjwa wachache wanaohitaji utaalamu wa juu zaidi kuwapeleka nchini
humo kwa ajili ya matibabu.
Tunaushirikiano
mzuri na nchi ya Israel kwani gharama za matibabu ya watoto hawa
zinagharamiwa na SACH. Licha ya Maafisa Wauguzi wawili kubaki nchini
humo kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo pia tuna madaktari bingwa wa
magonjwa ya moyo sita na wauguzi wawili ambao wamesoma nchini Israel
na hivi sasa wanatibu wagonjwa katika Taasisi yetu.Aidha Daktari wetu
mmoja bado anaendelea na masomo nchini humo.
Hili
ni kundi la tano la watoto kwenda kutibiwa magonjwa ya moyo nchini
Israel tangu mwaka 2015 ambapo Taasisi ya Moyo ilianza ushirikiano na
Taasisi ya Okoa Moyo wa Mtoto (Save a Child’s Heart –SACH) ya
kuwapeleka wagonjwa nchini humo. Hadi sasa watoto 46 wameshatibiwa
nchini humo na wanaendelea vizuri.
Taasisi
inaendelea kutoa wito kwa wazazi na walezi wasisahau kupima afya za
watoto wao pale watakapoona kuna hali ya tofauti katika ukuaji wa mtoto
kwani magonjwa mengi ya moyo yanaanzia utotoni. Mtoto akianza kuuguwa
magonjwa ya moyo wazazi wengi wanadhani ni matatizo ya kifua baada ya
kumfikisha mtoto Hospitali na kufanyiwa vipimo ndipo inagundulikwa kuwa
mtoto anasumbuliwa na magonjwa ya moyo.
Imetolewa na :
Kitengo cha Uhusiano na Masoko
Taasisi ya Moyo Jakaya Kikwete
11/12/2017
Post a Comment