Na Christina Mwagala
MSTAHIKI Meya wa Jiji la
Dar es Salaam Isaya Mwita ameondoka Jijini hapa jana jioni kuelekea
Addis Ababa, kuhudhuria mkutano wa kujadili changamoto zinazo wakabili
viongozi wa serikali za mitaa.
Mkutano huo wa siku tatu
umeandaliwa na Umoja wa Mataifa ambapo unalengo la kujadili na kutoa
majibu ya changamoto ambazo wanakutana nazo viongozi wa serikali za
mitaa wakiwepo Mameya wote.
Miongoni mwa changamoto
ambazo zitajadiliwa katika mkutamo huo pamoja na mambo mengine ni suala
la bajeti katika halmashauri na ukusaji wa mapato.
Mbali na Mameya ,mkutano huo pia utahudhuriwa na viongozi wengine wa serikali za mitaa kutoka Nchi mbalimbali.
Aidha Meya Mwita
atazungumza na mkutano huo kuelezea changamoto zilizopo katika jiji la
Dar es Salaam , namna ambavyo kwa asilimia kadhaa wameweza kuzitatua.
Aidha katika mkutano huo ataeleza pia mafanikio yaliyopo katika jiji la Dar es Salaam kupitia sekta mbalimbali za Maendeleo.
” Katika mkutano huo hatuta kuwa jiji la Dar es Salaam pekee
,ni Nchi mbalimbali Duniani zitakuwepo, tutajadili changamoto zinazo
tukabili kwenye halmshauri zetu, mafanikio,lakini pia kujengeana uwezo
kwenye utendaji kazi” alisema Meya Mwita.
Imetolewa leo Desemba 11
Na Christina Mwagala , Afisa Habari Ofisi ya Mstahiki Meya wa jiji
Post a Comment