Na Zephania
Klabu ya Borussia Dortmund leo tarehe 10 Novemba 2017, imeushangaza
ulimwengu wa soka baada ya kutangaza kumfukuza kazi kocha wake, Peter
Bosz na kumuajili Peter Stöger.
Peter Bosz amepoteza michezo 12 tangu ajiunge na klabu hiyo na kitu
pekee cha kushangaza ni kwamba Dortmund wamemuajili kocha ambaye
ametimuliwa na klabu ya inayoshika mkia wa ligi kuu nchini Ujerumani
Bundesliga.
Kuchaguliwa kwa Peter Stöger kumezua gumzo kubwa nchini Ujerumani
kwani wadau wengi wa soka wanasema Dortmund wamekosea kumsajili Kocha
ambaye mwenye historia mbaya kwenye kufundisha timu za Ujerumani.
Peter Stoger amepoteza mechi 8 na kupata sare 3 kabla ya kutimuliwa
na klabu ya FC Cologne ambayo inashika mkia kwenye msimamo wa
Bundesliga. Ambapo imeelezwa kuwa ndio kocha wa kwanza kuanza vibaya
kwenye tangu ligi hiyo ianzishwe.
Na hii inakuwa ni hatua ya kwanza kwenye historia ya Ligi kuu nchini
Ujerumani kwa kocha mwenye karba hiyo kuajiliwa na klabu kubwa nchini
humo.
Post a Comment