Na Yusuph Mwamba
SERIKALI
ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kupitia wakaguzi wake wa TRN imezipandisha vyeo vya Nyota nne zahanati tano baada ya kukidhi vigezo vya Serikali.
Akizungumza
na Gazeti hili, Diwani wa kata ya Vingunguti Omary Said Kumbilamoto,
amesema kuwa Manispaa ya Ilala kwa kuzingatia vigezo kupitia TRN imefanikisha
kuzipandisha zahanati tano moja wapo kati ya hizo ikiwa ni zahanati ya mtu
binafsi.
Miongoni
mwa zahanati hizozilizopandishwa vyeo vya nyota nne ni pamoja na Vingunguti, Tabata, Mongo landege, Kinyerezi,
Segerea pamoja na Kadlugambwa (p).
Aidha, kwa upande wa mwenyekiti wa zahanati hiyo, Nduze, amesema kuwa awali zahanati ya Vingunguti ilikuwa na nyota mbili wakati zilizobakia
zilikuwa na nyota tatu hivyo Vingunguti imepanda kwa nyota mbili.
Nduze,
amewashukuru wananchi kwa mawazo, maoni,
na changamoto walizokuwa nazo ambapo walizifanyia kazi na kupelekea kupanda kwa
nyota nne na kuwataka kuendeleza utamaduni wao wakuhakikisha wanafikia malengo
zaidi na waliyo nayo sasa.
Pia,
amempongeza kwa dhati Naibu Meya wa Halimashauri ya Manispaa ya Ilala, ambaye
ni diwani wa kata ya Vingunguti, Mh: Omary Said Kumbilamoto kwa kuwaongoza
vyema , ushauri na kutoa mchango wa hali na mali katika kufanikisha maendeleo
ya kata hiyo.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment