Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba

Zoezi la Upimaji wa Afya limeanza rasmi leo tokea 11 alfajiri kwenye Viwanja vya Mnazimmoja Jijini Dar es salaam,  huku tukishuhudia mamia ya wakazi kutoka sehemu mbali mbali wakijitokeza kupima afya zao kitu ambacho kimetia hamasa kwa kuitika wito wa Serikali ya Tanzania kupitia ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, RC Makonda ya kupima afya Bure.


Miongoni mwa malaengo ambayo RC Makonda , ameyataja ni pamoja na
Kujengea Wananchi utaratibu wa kupima Afya zao Mara kwa mara hata kama hawaumwi, Kusaidia wananchi wanyonge wanaotamani kupima Afya lakini hawana Uwezo wa Fedha kupata fursa ya kupima Afya, Kupunguza vifo   vitokanavyo na watu kutokujua historia ya Magonjwa yao hadi pale wanapougua.



Aidha  Makonda  amesema kila Mwananchi atakaefika kwenye Viwanja vya Mnazi Mmoja atapimwa na kupatiwa Matibabu Bure.



Amesema  Wananchi wengi wamekuwa wakipoteza maisha kutokana na kukosa utaratibu wa kupima Afya Mara kwa Mara na pindi wanapozidiwa na kufikishwa Hospital Ugonjwa unakuwa tayari umekuwa sugu hivyo kupoteza maisha.




Hata hivyo, RC Makonda amewapongeza    Madaktari na Wauguzi kutoka  Hospital za Umma, Jeshi na zile za Binafsi kwa kujitolea kumuunga mkono katika Kampeni hiyo ya kuokoa maisha ya binadamu kupitia vipimo vya afya.

Zoezi la upimaji Afya Bure litaendelea Kwenye Viwanja vya Mnazu Mmoja kwa muda wa siku tano kuanzia Asubuhi hadi Jioni ambapo ukomo wake utafanyika siku ya Jumapili Septemba 10.


JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.