Halloween party ideas 2015
Image




Na Florah Raphael

Makumbusho ya Taifa imeandaa onesho  la urithi wa kihistoria la "Fumo Liongo" iliyoandikwa na Prof. Emmanuel Mbogo ambapo wasanii kutokana kikundi cha "kaleleo" watashiriki  ikiwa ni mwendelezo wa programu ya sanaa inayoitwa "museum art explosion" inayofanyika kila ijumaa mwisho wa mwezi, mgeni rasmi katika onesho hilo anatarajiwa kuwa waziri wa habari na utamaduni, Sanaa na michezo Dk. Harrison Mwakyembe.
Akiongea Leo kwa niaba ya mkurugenzi mkuu wa Makumbusho ya taifa, mkuu wa idara ya programu hiyo chance ezekieli amesema kuwa lengo  kubwa la Makumbusho ya taifa ni kurithisha utamaduni wa mtanzania kwa vizazi vilivyopo na vijavyo pamoja na kuwapa nafasi wasanii nchini ya kuona na kujifunza njia bora ya uigizaji kwenye jukwaa.
Pia amebainisha faida zinazopatikana kutokana na mwendelezo wa "museum art explosion"na kusema kuwa zipo faida nyingi zilizopatikana lakini kubwa zaidi imeongeza mwamko wa wasanii kufanya kazi za maonyesho kwenye majukwaa pamoja na kuinua ari za wasanii kuendelea kufanya kazi za sanaa baada ya eneo zuri la kuonyeshea kazi zao.
Kwa upande wake muongozaji mkuu wa mchezo huo wa"Fumo Liongo" Ghonche materego amewashukuru Makumbusho ya Taifa kwa   kuwaalika kikundi kichanga cha "kaleleo" na kusema kuwa lengo lao kubwa ni kuhakikisha wanafufua tamaduni kubwa ambazo zimeonekana kufifia pamoja na kuwarithisha na kuwajenge uwezo wa kufanya maonyesho jukwaani vijana wanaochipukia.
Aidha Ghonche amesema kuwa wanajitahidi kurudisha utamaduni ndani ya jamii wa kwenda kutazama maonyesho ya sanaa kwenye majukwaa.
"Tunarudisha utamaduni wa kwenda kutazama maonyesho ya sanaa majukwaani"amesema Ghonche materego
Kuhusiana na suala la kufifia kwa michezo ya jukwaani Ghonche amesema kuwa sababu kubwa inayopelekea jambo hilo ni maslahi kutokana na kuanzishwa kwa runinga hivyo kupelekea wao kujipatia kipato kiurahisi.
Pia Ghonche ameongeza kuwa sababu nyingine inayopelekea maonyesho ya jukwaani kufifia ni kuwepo kwa ugumu wakupata kumbi za kufanyia mazoezi na maonyesho ambazo ni chache sana nchini.

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.