Na Yusuph Mwamba, Dar
MSANII mahili wa muziki wa uswazi maarufu kama Singeli, Aman
Hamis, kwa jina la usanii ‘Man Fongo’amefunguka baada ya kuachia ngoma yake
mpya ijulikanayo kwa jina la ’Pop cone mabisi’ akimshirikisha vyema msanii wa
miondoko ya RB, Ben Poul
Man Fongo, mzaliwa wa Dar es salam, anayetamba kwa
kibao chake cha ‘Hainaga ushemeji’alichomshirikisha mwana dada mtanashati
Shilole, hivi karibuni aliachia ngoma kali ambayo inaendelea kutamba hapa
mjini.
Katika harakati za kutaka kujua ni kwanini aliamua
kumshirikisha Ben Poul, Gazeti la Raia Tanzania lilifanya mahojiano naye katika
ofisi yake iliyopo Bamaga Makumbusho ili kujua historia yake kwa ufupi na
mafanikio yake
Man Fongo, alizaliwa tarehe 15/4/1992 mkoani Dar es
salaam, ni mtoto wa 7 kati ya watoto 8 wa mzee Hamis Kibwagale, alifanikiwa kuhitimu elimu yake ya msingi katika
shule ya msingi Kijitonyama Kisiwani mwaka 2008 na kufanikiwa kufaulu lakini
alishindwa kuendelea na elimu ya Sekondari kwa sababu binafsi ambayo hakutaka
kuitaja.
Akizungumza na Rai Tanzania, Man fongo alianza kuwa
DJ wa kupiga nyimbo za Singeli za uswahilini huku baadhi ya wasanii wa nyimbo hizo
wakimchukua kufanya mdananda pale wanapoalikwa, hivyo hakuwahi kufikiria kama
ipo siku atakuja kuwa msanii mkubwa licha ya yeye kuupenda mziki huo.
Wakati akiwa shule ya msingi, Man Fongo, alipenda
sana kuwa na kazi nzuri ya kuajiriwa Serikalini hivyo ikampelekea kuyapenda masomo ya sayansi lakini ndoto zake
hazikutimia hatimaye akaibukia katika tasnia ya muziki wa uswazi maarufu kama
Singeli ambapo mziki huo umetokea kuteka nyoyo za watu wengi hususani wakati wa
masherehe mbali mbali.
Aidha, Man Fongo, alianza kuingia katika tasnia ya
muziki wa Singeli rasmi mwaka 2006 kwa msukumo wa wasanii ambao alikuwa
akiwapigia nyimbo zao akiwa DJ, kwa kuwa wenzake walikuwa wakimuahidi kuondoka
nae kupiga nyimbo wakati wa kuondoka wanamuacha naye akaanza kupambana kwa
kutunga nyimbo zake mwenyewe na hatimaye akafanikiwa ndipo jina la Man Fongo
likipatikana kwa kutoa A katika Amani na kubakisha Man huku fongo liwa jina la
kitaa hakusita kulipokea jina hilo na kulitumia katika kazi zake za kisanaa.
Akifafanua kwa nini aliimba na mwana dada Shilole,
Man Fongo, alifunguka baada ya kusema kuwa Shilole ni msanii mkubwa sana kwa upande
wanawake,msanii ambaye hanaga majivuno hivyo kuimba nae kulimfanya ang’are sana
katika tasnia ya mziki wa uswazi maarufu
kama singeli kwa kuwa singeli ulikuwa haujashika kasi kama ulivyo sasa.
Kwa sasa msanii huyo aliyetamba na kibao cha
‘Hainaga ushemeji’ na sasa Pop cone mabisi , amefanikiwa kufikisha zaidi ya
albamu mbili , hivyo kudondosha kibao kipya ni kwa ajili ya kuwaburudisha wadau
wake na kuweza kuufanya muziki wa Singeli kupiga hatua kimataifa.
Hata hivyo, Man Fongo, hakusita kuzungumzia msanii
anayempenda katika tasnia hiyo ya muziki wa singeli baada ya nyota yake
kumdondokea Majid Migoma aliyetambaa kwa kibao chake cha ‘ mida ya kubeti’ kwa
kudai kuwa msanii huyo waliishi wote pamoja walipambana sana kuhangaikia tonge.
Fongo alienda mbali zaidi, huku akisema kwamba
katika nyimbo zake zote alizowahi kuzitoa nymbo moja tu ya ‘Safi tuu’
iliyotengenezwa na producer Yogo Beat ndiyo iliyogharimu kiasi kikubwa cha
fedha kwa upande wa video kwani ilimgharimu kiasi cha fedha za kitanzania Mil
4.5 lakini nyimbo zote zilikuwa kawaida pamoja na kuonekana kupendwa sana.
Kwa sasa msanii huyo ambaye ni kipenzi cha watu katika mziki wa singeli ,
anafanya kazi chini ya Menejimenti yake ijulikanyo kwa jina la Makers Entertainment
ambapo awali walikuwa na migogoro lakini
kwa sasa mambo yanaonekana kuwa mubashara.
Miongoni mwa changamoto alizowahi kukumbaana nazo ni
pamoja na kutokuwa na mawasiliano mazuri na Menejimenti yake ya Makers
Entertainment jambo lililompelkea kushuka chini pamoja na kutoa ngoma mpya
lakini hakufanikiwa kushika kasi kwa vile watu aliokuwa akifanya nao kazi
hawakuwa na nguvu za kuusogeza muziki huo hivyo kuamua kukaa chini kutatua
migogoro yao dhidi ya Menejimenti yake na hatimaye kuliamsha dude na Beb Poul.
Akizungumzia changamoto za jukwaani, Man Fongo,
ameenda mbali zaidi kwa kusema kuwa wadau muda wote wanahitaji kupagawishwa
hivyo kama msanii lazima awe na vitu tofauti tofauti vya kufanya wadau
wamuelewe na kufurahia show.
Akifunguka kuhusiana na kibao chake cha Hainaga ushemeji, alisema wimbo huo aliutunga
kutokana na kuwepo kwa matukio hayo mtaani hivyo kama msanii lazima abadilike
kutokana na wakati na mazingira halisi ili kuelezea jamii na kuhabarisha jamii
matendo yapo na yanafanyika kwahiyo haikuwa jambo rahisi kutungunga nyimbo kama
hivyo.
Akizungumzia uwezo wa ma-producer, Man Fongo,
amemwagia sifa kede kede Producer mbunifu Abi dad ambaye ambaye ametokea
kuwa ni kipenzi cha watu kutokana na
ubunifu wake aliyetengeneza ngoma kadhaa za wasanii nguli hapa nchini ikiwemo Ally Kiba, Christian Bella pamoja na
Kassim Mganga.
Kwanini kundi lake halina wanawake, Man Fongo
amefunguka na kusema muziki huo unaonekana na watu wengi sana, na wanume
wanauvaa uhusika wa wanawake, akiwa mwanamke ataanza kucheza na kumwaga radhi
lakini mwanaume nae atakatika viuono na kuubeba uhusika wa mwanamke hivyo
watazamaji watasema anacheza kama mwanmke kwa mantiki hiyo mwanamke anakuwa
hana kazi tena.
Mpaka sasa mafanaikio aliyoyapata tangia aingie
katika muziki huo wa singeli ni pamoja na kusafiri nchi za nje kama vile India
katika miji ya Bangaloo pamoja na Newdehl kwa ajili ya show akiambatana na
mwana dada Shilole, kupata tuzo ya msanii chipukizi mwaka 2016, mbali na hayo
pia amaefanikiwa kufunga ndoa 2016 katika fungo
na sasa anatarajiwa kuitwa baba ifikapo mwezi wa 3 mungu akipenda, kanunua kiwanja kilichopo Saranga Kimara ,
gari aina ya Voxy wagen new model, kushiriki katiaka fiesta 2016 akiwa pamoja
na Wizkid, nyama choma Festival, hivyo anaendelea kula bata kwa kile
alichokivuna.
Kuhusu msanii anayemuumiza kichwa katika singeli,
Man Fongo amefunguka baada ya kusema kuwa hajaona msanii wa kumsumbua kwani
yeye ni msanii pekee wa singeli aliyesafiri nje ya nchi, mwenye tuzo hivyo kama
watatokea wasanii wenye CV za aiana yake ndipo atamtaja msanii anaye muumiza
kichwa .
Kufanya ngoma na Ben Poul, Man Fongo, amesema kuwa
Ben Poul, ni msanii mkubwa sana anayetambulika kimataifa hivyo kufanya muziki na msanii huyo
kutamfanya nae aweze kutambulika kimataifa hivyo wadau wa Ben Poul wakisikia
ngoma yake watapenda kusikiliza hivyo kuufanya mziki wa singeli kuwa
wakimataifa kama ulivyo kwa muziki mwengine kama vile Hip hop au Bongo Fleva, wadau
wanataka ujumbe tofauti tofauti na ujazo wake hivyo ana anaamini Ben Poul atamsaidia
kumtangaza Kimataifa.
Mpaka sasa Man Fongo, ameachia ngoma kali
ijulikanayo Pop cone mabisi wenye ujumbe wa kuwahamasisha vijana wafanye kazi
waondokane na utegemezi na njia za haramu za kujipatia fedha kama vile kubaka,
kuuza dawa za kulevya kwani wakifanya biashara ndogo ndogo zitawasaidia kukimu
mahitaji yao na hatimaye kusonga mbele kimaisha, pia amepongeza hatuaza vijana
kuchipukia katika mziki huo wa singeli kwamba unaleta hamasa na changamoto
katika tasnia hiyo ya nymbo za singeli.
Ushauri kwa Serikali, na wadau wengine, amesema kuwa
singeli ni mziki wa kinyumbani, chimbuko la kitanzania hivyo lazima upewe
kipaumbele kama ilivyo kwa mizki mingine hapa nchini ili kujivunia asili ya
kitanzania.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment