Na Yusuph Mwamba, Dar
BAADA ya kumalizika kwa msimu wa ligi kuu ya Tanzania bara (Vodacom) 2016/2017 huku Dar es salaam Young Africans ikifanikiwa kuibuka kidedea mara tatu mfululizo wakiwaacha watani zao Simba kushika nafasi ya pili huku wakifanikiwa kutwaa kombe la FA, sasa ni waakati wa kujiandaa na msimu mpya wa ligi kuu unaotegemewa kuanza kutimua vumbi Mwezi September mwaka huu baada ya pazia la usajili kufungwa .
Msimu uliopita tulishuhudia timu tatu zikishuka daraja, miongoni mwa timu hizo ni pamoja na African Lyon ya Dar Es Salaam , Toto African ya Mwanza na JKT Ruvu ya mkoani Pwani.
Wakati tukisubiri hadi msimu mpya wa ligi kuu ya Vodacom kuanza kutimua vumbi ni vizuri tukazifahamu kwa undani vilabu ambavyo vimepanda daraja ili kuweza kubaini mapungufu yao na kutabiri nani anaweza kushuka au wote wakasalia katika msimu ujao wa mwaka 2017/2018.
Singida United
Hii ni timu ambayo inapewa nafasi ya kuweka Historia kwa kupanda ligi kuu na kuchukua ubingwa wa ligi kuu .
Singida United, inapanda ligi kuu baada ya kukaa takribani miaka 17 bila kuionja ligi hivyo . Kuna kila dalili klabu hiyo ya watoto wa Singida kuwasumbua vigogo na kuleta changamoto katika msimu mpya wa ligi kuu .
Kingine kitakachoifanya Singida United itambe msimu ujao ni udhamini wa shilingi milioni 250 kutoka kwa wadhamini wa mchezp wa kubashiri Sports Pesa, kwa kipindi cha miaka mitano walioupata kutoka kwa Kampuni ya Michezo ya Kubashiri ya Sportpesa.
Mkataba huu pia utaipa Singida United bonus nyingine kama watachukua ubingwa wa Ligi Kuu Bara au Kombe la Kagame au ubingwa wa Afrika
Ukiachilia udhamini walio upata imani nyingine ni pale ilipoingia kandarasi na aliyekuwa mkurugenzi wa ufundi na kocha wa zamani wa Yanga, Mholanzi , Hans Pluijm .
Akiwa kunako klabu ya soka ya Yanga , Pluijm, aliweza kuisaidia timu hiyo kuwa bingwa wa ligi kuu Tanzania bara mara mbili mfululizo tangu msimu wa 2014/15 na 2015/16 pamoja na kushiriki hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika
Katika
kujiimarisha vyema na mikikimikik ya ligi kuu ya Vodacom , Klabu ya Singida
United ,mpaka sasa imeshanasa saini ya wanandinga saba wa kimataifa kutoka
mataifa mbali mbali, miongoni mwa wachezaji hao ni pamoja na Michelle Katsvairo Twafadhwa Kutinyu(Zimbabwe) , Elisha
Muroiwa kutoka Zimbabwe (27),Wisdom Mtasa raia wa Zimbabwe (22) , Dany Usengimana(
Rwanda) , Shafik Batambuze (Uganda), Michael Rusheshangonga(Rwanda) , Batambuze
na Nhivi( Zimbabwe), wakati wachezaji wa ndani ni Deus Kaseke kutoka Yanga,
Kigi Makassy (Ndanda FC), Atupele Green (JK Ruvu), Miraji Adam (African Lyion),
Kenny Ally (Mbea City), Ally Mustapha ( Yanga) Salum Chuku ( Toto Africa).
Lipuli FC yenye maskani yak Mkoa wa Iringa ndiyo iliyokuwa timu ya kwanza kupanda Ligi Kuu Bara kwa msimu ujao wa 2017-2018 baada ya kushika nafasi ya kwanza kwenye kundi A la ligi daraja la kwanza.
Lipuli FC inarejea kwenye ligi kuu Tanzania bara baada ya kupita zaidi ya miaka 13 tangu iliposhuka daraja miaka ya mwanzoni mwa 2000.
Lipuli
FC inaingia kwenye ligi kuu Tanzania bara ikiwa na changamoto ya kiuongozi
baada ya viongozi wake kuingia kwenye mgogoro wa kiongozi hali iliyofanya Chama
cha mpira mkoani Iringa (IRFA) kuichukua timu na kuunda kamati ya kuisimamia .
Njombe Mji inapanda Ligi Kuu kutoka kundi B baada ya kuifunga Mafinga goli 2 – 0 na kufikisha pointi 22 ambazo wapinzani wake , klabu za KMC, Polisi Morogoro na JKT Mlale wasingeweza kuzifikia .
Tayari uongozi wa
chama cha soka mkoani Njombe (NJOREFA) umeahidi kukarabati uwanja wa Sabasaba
ili kuruhusu mechi za ligi kuu zipigwe kwenye uwanja huo .
Kwa
mantiki hiyo, ni bora timu hizi zikajiepusha na dhambi za vigogo wa soka hapa
nchini ili ziweze kufikia maendeleo na kubakia kwenye ligi hiyo jambao ambalo
litasaidia kupata wadhamni watakao saidia maendeleo ya soka na vilabu vyao.
Dhambi
ambazo wanatakiwa kujiepusha nazo ni pamoja na kuepuka kupanga matokeo,
kutowaogopa vigogo, viongozi kuwa makini na utunzaji wa kumbu kumbukumbu za
wachezaji wanapopata kadi viwanjani na kutojiingiza katika migogoro binafsi na
chama cha soka cha TFF ili kulinda hadhi zao.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment