Na Yusuph Mwamba
TABIA hujenga mazoe, miaka ya nyuma tulikuwa
tukiwaona Real Madrid, Barceleona , Manchester City pamoja na Chlsea
wakitambiana kwa matumizi makubwa ya
pesa pindi inapokaribia majira ya usajiri kwa wachezaji, lakini mwaka huu
tumeshuhudia Ufaransa nako wakijaribu kuwatambia vigogo wa Hispainia kwa
kumwaga mpunga mkubwa baada ya klabu ya soka ya PSG kumnyakua nyota wa zamani
wa Barcelona Neyar kwa mkwanja marefu na
kuweka rekodi Duniani.
Baada ya PSG kuonesha umwamba wao hebu tuangalie
wanandinga wengine wanaongoza kwa kulipwa dau kubwa katika uhamisho kutoka
kwenye vilabu vyao
1.
Neymar JR
Huyu ndiye staa
anayeongoza kusajliwa kwa pesa nyingi zaidi miongoni mwa mastaa wote
duniani.Neymar (25) ambaye alikipiga klabu ya Barcelona kwa mafanikio makubwa,
alisajiliwa kwa dau la Paundi milioni 220 kutoka klabu ya soka ya Barcelona
kwenda PSG ndiye aliyepiga mkwanja mrefu kuliko wote Duniani.
2.Paul Pogba
(24)
Kiungo huyo anafuatia kwa kushika namba mbili, baada ya kunyakua kiasi cha paundi milioni 105 akitokea klabu ya Juventus kwenda klabu ya Manchester United.
3.Gareth Bale
Bale (28) raia wa
Walesi, nafasi yake ni mshambuliaji, alisajiliwa kwa dau la Paundi milioni 100
akitokea klabu ya soka ya Tottenham Spurs kwenda Real Madrid, mafanikio yake ni
makubwa huku akicheza pamoja na Christiano Ronaldo
4.Christiano Ronaldo
Ronaldo (32) alisajiliwa
kwa dau la paundi milioni 94, alitokea klabu ya soka ya Manchester United
kwenda Real Madrid kwa sasa ndiye lulu wa klabu hiyo licha ya kusajiliwa kwa
dau hilo lakini ana miliki mali za maana.
5.Gonzalo Higuan (30)
Mshambuliaji mzuri
mwenye uwezo wa kufunga alisajiliwa kwa dau la paundi milioni 90 akitoke kla bu
ya soka ya Napoli na kujiunga na klabu ya soka ya Juventus zote za Italia
6.Romelu Lukaku (24)
Huyu ni lulu kwa sassa,
alikuwa mfungaji bora ligi kuu ya Uingereza msimu uliopita, alichezea klabu ya
Evertoni kwa mafanikio makubwa sana, alisajiliwa kwa dau la Paundi milioni 85
kutoka Everton kwenda Mnchester Unitd.
7.Luis Suarez
Suarez (30) raia wa
Uruguay, ni mtukutu akiwa uwanjani lakini ni mchezaji mzuri ambaye muda wowote
anaweza kubadilisha matokeo, alisajiliwa kutoka klabu ya Liverpool kwa dau la
Paundi milioni 82.3 kwenda Barcelon mpaka sasa amefanikiwa kucheza jumla ya
michezo 120 na kufunga jumla ya magoli 100 akiwa nyuma ya Mess
8.James Redriguez (26)
Ni mchezaji mzuri japo
hajapata namba maalumu lakini anauwezo wa kufunga, alisajiliwa kwa dau la
paundi milioni 79.8 akitokea klabu ya
Monaco kwenda klabu ya Real Madrid
9.Zinedine Zidane ( 45)
Fundi wa mpira,
alishakuwa mtawala wa Dunia miaka iliyopita pamoja na mataji mengi aliyoyapata alisaidia sana Taifa lake la Ufaransa katika
mchuano mbalimbali ya Kombe la Dunia na ile ya Ulaya, mafanaikio
hayo ndiyo yaliyomfanya mpaka leo kukiongoza vyema kikosi cha Real Madrid na
kufanikiwa kuchukua kombe la ligi na klabu Bingwa barani Ulaya 2016/2017, alisajiliwa
kwa dau la paundi milioni 77.5 kutoka klabu ya Juventus kwenda Real Madridi
10.Angel Di Maria (29)
Huyu ndio anakamailisha
orodha ya wanandinga walisajiliwa kwa mkwanja mrefu Duniani, alisajiliwa kwa
ada ya Paundi milioni 75.6 akitokea klabu ya Real Madrid kwenda Manchester
United
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment