Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba
MKUU  wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, amefanya mkutano wa  Kongamano la tathimini ya hali ya miundombinu ya Barabara kwenye Mkoa wake katika ukumbi wa mwalimu nyerere Jijini Dar es salaam.
 

Katika Kongamano hilo Wananchi wamepata nafasi ya kuelezea kero za Barabara katika maeneo yao na kupatiwa majibu na Wataalamu wa Barabara ambapo kumekuwa na maswali mbali mbali ya wachangiaji wa maada kutoka sehemu tofauti tofauti na kupatiwa ufumbuzi wa maswali yao na wataalamu waliofika japo hayakurdhishwa sana na mkuu wa mkoa.

 RC Makonda  amewaagiza Wakuu wa Wilaya zote kuhakikisha wanasimamia imara ujenzi wa Barabara zinazojengwa katika bajeti iliyotengwa kwaajili ya barabara katika mwaka wa fedha 2017/2018 ili kuhakikisha Barabara zinakuwa za viwango bora vyenye kukidhi mahitaji ya wananchi na jamii kwa ujumla.

Licha ya wataalamu kujielezea lakini mkuu wa mkoa hakuridhishwa na majibu yao kwani kila jawabu na kero zilizokuwa zinatolewa baadhi ya viongozi waliohudhuria walipingana na na majibu yao.

Mbali na kutoridhishwa na utendaji wa wakandarasi pamoja na makampuni yanayofanya tenda ya utengenezaji wa bara bara, lakini  ameendelea kushikilia msimamo wa kutoruhusu Kampuni za ujenzi za Del Monte na Skol Building Contractionkufanya kazi katika Mkoa wake.

 Katika uchunguzi alioufanya Makonda amebaini ya Makampuni ya ujenzi yanayoazima vifaa kutoka kampuni nyingine ili waweze kupatiwa usajili na pindi wanapopewa tenda ya ujenzi hujikuta wanakosa vifaa na wataalamu hali inayopelekea ujenzi chini ya kiwango na kuchelewa kukamilika.


JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline



Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.