WAKILI wa utetezi katika kesi inayomkabili mfanyabiashara Yusuf Manji ya kutumia madawa ya kulevya, Hoodson Ntisiepo, amemuuliza mtoa ushahidi kutoka ofisi ya mkemia mkuu wa serikali iwapo mkojo alioupima ulikuwa ni Manji au wa polisi?
Hayo amehoji leo Jumatano, Agosti 23 katika Mahakama ya Kisutu, wakati wa kusikilizwa kwa ushahidi wa kesi hiyo.
Wakili huyo alihoji jambo hilo ili
mashahidi waithibitishie mahakama kwani wakati Manji anakwenda msalani
kutoa sampuli hiyo ya mkojo aliongozana na askari, jambo ambalo
lilifanya wasikilizaji wa kesi hiyo waangue vicheko ndani ya mahakama.
Kesi hiyo ilikuwa imekuja kwa ajili ya
kutolewa ushahidi na imeahirishwa hadi Agosti 25 mwaka huu ambapo Hakimu
anayesikiliza kesi hiyo Cyprian Mkeha atakapotoa uamuzi kama mshitakiwa
ana kesi ya kujibu ama la.
Ofisa kutoka ofisi ya mkemia wa serikali
ambaye alikuwa akitoa ushahidi wake ameelezea namna alivyopima mkojo
huo na kugundulika kuwa na chembechembe za madawa aina ya heroine
ambapo.
Pia aliieleza mahakama kuwa majibu ya
vipimo hivyo yanaweza kutokana na matumizi mbalimbali ya dawa zikiwemo
dawa za binadamu za usingizi.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment