Mkurugenzi Mkuu wa Idara ya Habari, Maelezo na Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi amewataka wamiliki wa magazeti na majarida mbalimbali kufanya hima kuenda kujisali upya kuanzia leo kwani wasipofanya hivyo watashindwa kuendelea kuchapisha.
Dkt. Abbasi amebainisha hayo kwenye
mkutano wake na waandishi wa habari na kusema endapo chombo chochote
kitakaidi agizo hilo mpaka kufikia Oktoba 15 mwaka huu basi litakuwa
linatenda kosa la jinai
"Kuanzia leo hadi Oktoba 15 mwaka huu
magazeti yote yahakikishe yanakuja kusajiliwa upya katika mfumo wa mpya
wa utoaji wa leseni kwa machapisho yote. Mfumo mpya wa utoaji leseni ni
muendelezo wa azma yetu ya kuifanya tasnia ya habari kuwa
taaluma",alisema Dkt. Abbasi.
Pamoja na hayo, Dkt. Abbasi aliendelea
kwa kusema "baada ya Oktoba 15 mwaka huu halitaruhusiwa gazeti au jarida
kuendelea kuchapisha bila ya kuwa na usajili huu mpya wa leseni".
Mbali na hilo, Dkt. Abbasi amewakumbusha
wanahabari ambao wapo chini kielimu kuhakikisha kwamba katika miaka
mitano waliopewa wanafikia kiwango kilicho wekwa cha taaluma kwa
wanahabari hao.
"Katika taaluma ya habari kwa wanahabari
tumeweka miaka 5 wajiendeleze, wale ambao wapo chini ya Diploma
wakajiendeleze", alisema Dkt. Abbasi.
Kwa upande mwingine, Dkt. Abbasi amesema
kwa mujibu wa sheria vyombo vyote vitasajiliwa upya bila ya kujali kama
ni jarida la Wizara au gazeti la serikali.
Dkt. Abbasi amebainisha hayo kwenye
mkutano wake na waandishi wa habari na kusema endapo chombo chochote
kitakaidi agizo hilo mpaka kufikia Oktoba 15 mwaka huu basi litakuwa
linatenda kosa la jinai.
"Kuanzia leo hadi Oktoba 15 mwaka huu
magazeti yote yahakikishe yanakuja kusajiliwa upya katika mfumo wa mpya
wa utoaji wa leseni kwa machapisho yote. Mfumo mpya wa utoaji leseni ni
muendelezo wa azma yetu ya kuifanya tasnia ya habari kuwa
taaluma",alisema Dkt. Abbasi.
Pamoja na hayo, Dkt. Abbasi aliendelea
kwa kusema "baada ya Oktoba 15 mwaka huu halitaruhusiwa gazeti au jarida
kuendelea kuchapisha bila ya kuwa na usajili huu mpya wa leseni".
Mbali na hilo, Dkt. Abbasi amewakumbusha
wanahabari ambao wapo chini kielimu kuhakikisha kwamba katika miaka
mitano waliopewa wanafikia kiwango kilicho wekwa cha taaluma kwa
wanahabari hao.
"Katika taaluma ya habari kwa wanahabari
tumeweka miaka 5 wajiendeleze, wale ambao wapo chini ya Diploma
wakajiendeleze", alisema Dkt. Abbasi.
Kwa upande mwingine, Dkt. Abbasi amesema
kwa mujibu wa sheria vyombo vyote vitasajiliwa upya bila ya kujali kama
ni jarida la Wizara au gazeti la serikali.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment