Na Yusuph Mwamba
MSTAHIKI Meya wa Jiji la
Dar es Salaam Isaya Mwita amesema kuwa jiji linatarajia kulikabidhi jengo la
Machinga Complex Mfuko wa Taifa wa Hifadhi ya jamii (NSSF), ili iweze
kuliendesha na kurejesha fedha zilizotolewa na mfuko huo kama mkopo kwa
halmashauri ya jiji kwa ajili ya ujenzi wa jingo hilo.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini hapa leo, Meya Mwita amesema kuwa halmashauri iliingia mkataba na
NSSF wa mkopo wa shilingi bilioni 10 kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo .
Ameongeza kuwa katika hatua za
ujenzi huo, mkataba ulifanyiwa nyongeza ya shilingi bilioni 2.14 na hivyo
kufikia jumla ya mkopo wa shilingi bilioni 12.14 lakini hata hivyo makabidhiano
ya jengo hilo yalipofanyika mwaka 2010 gharama za ujenzi zilifikia bilioni
12.7.
“ Kinachonishangaza na kuniogopesha
ni kwamba , tumejulishwa kuwa deni hilo hivi sasa linakadiriwa kuwa zaidi ya
shilingi bilioni 40, kwakuwa tumejirizisha kwamba hatuna uhalali wa deni hilo,
nasema hivi, jengo hili nitalikabidhi kwa NSSF, waliendeshe wao, na kurejesha
fedha za mkopo ambazo walichukua” amesema Meya Mwita.
Amefafanua kuwa kwa mujibu wa
mkataba wa jengo hilo, lilipaswa kuwa na ghorofa tano upande mmoja , ghorofa
sita upande mwingine sambamba na kuhudumia wafanyabiashara wadogo wa dogo 10,
000 lakini chakushangaza NSSF walifanya tofauti na mkataba huo.
Amesema wakati wanakabidhi jengo
hilo lilikuwa na ghorofa nne lenye uwezo wa kuchukua wafanyabiashara 4,206
jambo ambalo imefanya jiji kushindwa kufikia malengo yake ya ulipaji wa deni
hilo na utoaji huduma kwa walengwa.
Meya Mwita alifika mbali zaidi na
kusema kuwa, halmashauri ya jiji haikuhusika na usimamizi wa fedha zilizokopwa
na kufanya kushindwa kuthibitisha gharama zilizotumika.
“ Mkataba wetu uliitaka NSSF kutoa
fedha kwa halmashauri ya jiji kwa ajili ya ujenzi wa jengo hilo, jambo
ambalo halikufanyika, fedha zilizoongezeka kutoka bilioni 12.14 hadi kufikia
bilioni 12.7 ziliongezwa bila kufikia makubaliano yoyote kati ya jiji na NSSF”
alifafanua Meya Mwita.
Hata hivyo Meya Mwita alisema kwa
muda mrefu jiji limekuwa likijaribu kutafuta muafaka na NSSF kuhusu namna ya
ulipaji kodi jambo ambalo halikufanikiwa na kusisitiza kwamba , kamwe jiji
halitalipa deni hilo kwakuwa haina uwezo wakulilipa.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment