Na Mwandishi wetu
WAZIRI MKUU
Kassim Majaliwa amekutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Shirika la
Viwanda vya Sukari nchini Cuba, Bw. Francisco Lled, ambaye amekubali
kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika kuongeza uzalishaji wa
sukari nchini.
Shirika la
Sukari la nchini Cuba linauwezo wa kuzalisha tani milioni nne za sukari
kwa mwaka huku mahitaji ya ndani ni tani 700,000, ambapo kiasi
kinachobaki huuzwa nje ya nchi. Kwa sasa shirika hilo linazalisha tani
milioni mbili tu katika viwanda vyake 56.
Waziri Mkuu
alikutana na Bw. Lled Alhamisi, Agosti 24, 2017, wakati alipofanya ziara
katika kiwanda cha kuzalisha sukari cha UGB Central Azucarero 30 de
Noviembre katika mji wa San Nicola’s de Bari ambacho ni kati ya viwanda
27 vya shirika hilo linalomilikiwa na Serikali ya Cuba kwa asilimia 100.
Katika
mazungumzo yao Waziri Mkuu alimshawishi Bw. Lled kuja nchini kwa ajili
ya kuwekeza katika ujenzi wa viwanda vya kuzalisha sukari. Alisema kwa
sasa Tanzania kuna viwanda vikubwa vitano vya sukari ambavyo uzalishaji
wake hautoshelezi mahitaji ya ndani.
Waziri Mkuu
alivitaja viwanda hivyo ambavyo ni Mtibwa na Kilombero (Morogoro),
Mahonda (Zanzibar), TPC (Kilimanjaro) na Kagera ambavyo vyote
vinazalisha jumla ya tani 320,000 za sukari kwa mwaka huku mahitaji
yakiwa ni zaidi ya tani 400,000.
Hata hivyo,
Waziri Mkuu alisema Serikali kwa kushirikiana na sekta binafsi
inatarajia kujenga viwanda vitatu vya kuzalisha sukari, ambavyo
vitazalisha sukari itakayotosheleza mahitaji na ndani ya nchi na kiasi
kitakachosalia kitauzwa nje.
Kwa upande
wake Bw. Lled alisema sera za Cuba haziruhusu shirika kwenda kuwekeza
nje ya nchi na badala yake wanaruhusiwa kuzisaidia nchi zinazohitaji
kujenga viwanda hivyo kwa kutoa ushauri na usimamizi wa ujenzi wa miradi
hiyo.
Alisema
Shirika lake lipo tayari kushirikiana na Serikali ya Tanzania katika
usimamizi na kutoa ushauri wa ujenzi wa miradi ya viwanda vya kuzalisha
sukari na kwamba walishatoa huduma kama hiyo katika nchi mbalimbali
zikiwemo Brazil na Bolivia.
Katika hatua
nyingine, Bw. Lled alisema mbali na uzalishaji sukari pia shirika hilo
kupitia viwanda vyake vya sukari wanazalisha vyakula vya mifugo, asali
ambayo inatumika katika viwanda vya kutengeneza vinywaji vikali pamoja
nishati ya umeme.
Alisema miwa
ya kuzalishia sukari katika viwanda vyao wanaipata kutoka kwenye vikundi
vya ushirika wa kulima wa miwa vilivyoko katika mikoa yote nchi nzima
kasoro mkoa wa Havana na Pañar del Rio na kwa mkulima mmoja mmoja ambao
kwa pamoja hukusanya miwa katika vituo ambavyo hupeleka kiwandani.
Hata hivyo
alisema kuwa viwanda vyao vinanunua miwa kwa bei tofauti kulingana na
ubora wa miwa na kwamba shirika lao linawasaidia wakulima kwa
kuwaelimisha namna bora ya kulima pamoja na kuwaazima mashine za kuvunia
wakati wa mavuno. Miwa yote nchini Cuba inavunwa kwa kutumia mashine.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment