Na Mwandishi wetu
Upande wa
utetezi umeiomba Mahakama kuulazimisha upande wa mashtaka kuifuta kesi
ya utakatishaji fedha, inayomkabili aliyekuwa Kamishna Mkuu wa TRA,
Harry Kitilya na wenzake.
Wakili wa
utetezi, Majura Magafu ametoa ombi hilo jana katika Mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu Mbele ya Hakimu Mfawidhi Cyprian Mkeha wakati kesii hiyo
ilipokuja kwa kutajwa.
Aliiomba
mahakama kuwa, upande wa mashtaka ulazimishwe kesi ifutwe ama waiondoe
mahakamani kwa sababu washtakiwa awali walikuwa chini ya dhamana na
wakiripoti kila walipohitajika Takukuru.
Wakili wa utetezi, Majula Magafu alidai kuwa sasa imefikia wakati mahakama ihakikishe maelekezo inayoyatoa yanaheshimiwa
"Mahakama
inaweza kuifuta kesi ili ushahidi ukikamilika waletwe tena, kwa sababu
imebaki hadithi kila wakija wanasema wanasubiri vielelezo kutoka Ulaya
na miaka inaenda tu,".
Akijibu hayo,
wakili wa serikali, Constantine Kakula alidai upelelezi wa kesi hiyo
unashindwa kukamilika kwa sababu inahusisha uchunguzi unaovuka mipaka.
Alidai, siyo
kama jamhuri imelala bali inafanya mawasiliano na upande wa pili, kwa
sababu hatuwezi kumlazimisha anayetuma nyaraka za upelelezi kutoka
Ulaya.
Hakimu Mkeha akautaka upande wa mashtaka kuhakikisha unakamilisha upelelezi.
Kitilya na
wenzake, aliyekuwa Miss Tanzania mwaka 1996, Shose Sinare na Sioi
Solomon wanashtakiwa kwa utakatishaji wa fedha dola milioni 6. Kesi hiyo
imeahirishwa hadi September 8/2017.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment