Na Yusuph Mwamba
MLINZI wa kati wa Kimataifa wa Austria, Kevin Wimmer, amefanikiwa kuongeza mkataba na klabu ya soka ya Tottenham kwa kandarasi ya miaka mitano katika kutumikia klabu hiyo kwa mara nyingine tena .
Wimmer mwenye umri wa miaka 23, ameongeza makataba na klabu ya Tottenham kwa miaka mitano huku awali akikipiga kunako klabu ya soka ya soka ya FC Koln huku akiwa huru ambapo uhamisho wake umegharimu kiasicha fedha taslimu Euro milioni 4 ambapo mkataba wake unatarajia kumalizika mwaka 20121.
"Ninafuraha kubwa kubaki kunako klabu yangu ,japo msimu wangu wa kwanza ulikuwa mzuri sana kwangu naamini changamoto zilizopo nitaweza kukabiliana nazo,pia naamini ndoto zangu zimekamilika, lakini sitapenda niishie hapa bali nitajitahidi kuonesha uwezo zaidi ili niweze kufika mbali zaidi na hapa".Alisema Summer
"Nilimpigia simu mama angu kwa kuwa amekuwa mstari wa mbelekuona nafanikiwa na amenipa baraka zote kuweza kusalia kunako klabu hii, ninafuraha sana na wazazi wangu wamefurahia maamuzi yangu, naamini kujifunza kwangu kila siku nitafanikiwa japo msimu ni mrefu nitapambana". Aliongeza Wimmer
Mwanandinga huyo, kabla ya kujiunga na klabu ya FC Koln, alishawahi kuichezea klabu ya soka ya LASK Linz iliyopo Nchini Austria kabla ya kujiunga na FC Koln mwaka 2012 na kufanikiwa kucheza jumala ya michezo 32 katika ligi ya Bundesliga.
Msimu uliopita,Wimmer , alifanikiwa kucheza jumla ya michezo 21 katika michezo hiyo, jumla ya michezo tisa ametumikia kunako ligi kuu na michezo sita Europa League.
Kusalia kwa Wimmer, kutamfanya mwanandinga huyo kuchukua nafasi ya Jan Vertonghen aliyepata majeraha msimu uliopita na ameanza kampeni ya kujiwinda na ligi kuu ya Uingereza akiwa kama beki wa kushoto baada ya Vertonghen kujitonesha jeraha tena akiwa na timu yake ya Taifa ya Ubelgij katika michuano ya fainali ya Euro 2016 iliyomalizika hivi karibuni huko Ufaransa.
Post a Comment