Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Wastoto Ummy Mwalimu katika wakati akizindua Maabara
Na Mariamu Muhando Dar es salaam
Mamlaka ya chakula na
Dawa Tanzania -TFDA imetakiwa
kuendelea kuwajengea uwezo Wataalamu wa Maabara ndogo Hamishika wanaohusika na
uchunguzi kupitia maabara hizo ili kuendana na mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia.
Wito huo umetolewa na Waziri
wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Wastoto Ummy Mwalimu katika kuzindua
Maabara Hamishika kumi zenye thamani ya
shilingi milioni mia moja zitakazotumika katika mikoa mbalimbali nchini.
Akizungumza katika uzinduzi
huo Waziri Ummy amesema lengo la kunua maabara hizo ni kuimarisha nguvu katika uchunguzi wa haraka na
wa awali wa dawa na kudhibiti ubora na usalama wa dawa zinazoingia nchini na
zilizo katika masoko
Nae Mkurugenzi Mkuu wa
Mlaka ya Chakula na Dawa TFDA Hitti B. Sillo
amesema Maabara hizo zimepangwa kupelekwa katika ofisi tatu za kanda ya TFDA
ikiwemo Mbeya, Mtwara, na Dar es salaam.
Mamlaka ya Chakula na
Dawa TFDA Inajukumu la kudhibiti ubora, Usalama na ufanisi wa bidhaa za
chakula, dawa, Vipodozi, vifaa tiba na vitendanishi ili kulinda afya ya jamii
dhidi ya madhara yanayoweza kutokea kutokana na matumizi
ya bidhaa duni na bandia.
Post a Comment