Na Issa Ramadhani
KLABU ya Soka ya Manchester United, ipo mbioni kuinasa saini ya Mlinzi wa Kimaitaifa wa Timu ya Taifa ya Jamhuri ya Ireland, anyekipiga kunako klabu ya soka ya Everton, Seamus Coleman.
Seamus Coleman, ambaye ni nahodha wa Timu ya Taifa ya Jamhuri ya Ireland inasemekana kuwa alikuwa katika mipango ya muda mrefu na klabu ya United.
Aidha, pamoja na kupewa kipaumbele kwa mlinzi huyo kujiunga na kikosi cha Manchester United, lakini Meneja wa klabu hiyo, Jose Mourinho, amekiri baada ya kusema kuwa beke wa kati ni tatizo kwa klabu hiyo.
Licha ya kuitaji huduma ya mlinzi huyo wa kati wa klabu ya Everton, lakini matarajio yake mengine ni kuona mlinzi wa kati wa klabu ya soka ya Monaco ya Ufaransa, Fabinho anajiunga na Mashetani hao.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment