Na Yusuph Mwamba
WAKATI maadhimisho ya siku ya Saccos Duniani yakiwa katika kilele cha kuhitimisha maadhimisho hayo, tulishuhudia mambo maonesho kadha wa kadha lakini kikubwa zaidi ni pale tuliposhuhudia waandalizi wa maadhimisho hayo kwa kuwawezesha na kuwatunuku vyeti pamoja na zawadi kwa wale waliofanya vizuri zaidi licha ya wote kufanya vyema lakini kwenye mshindani hapakosi mshindi.
Miongoni mwa Saccos zilizo jikusanyia ushindi huo ni pamoja na TANESCO SACCOS, ambao walifanikiwa kuchukua nafasi ya kwanza, huku NDUGUMBI COMMUNITY SACCOS wakibeba tuzo hiyo baada ya kushika nafasi ya pili wakifuatiwa na BANDARI SACCOS wakishika nafasi ya tatu.
Ndugumbi Community Saccos ni chama cha Akiba na Mikopo (SACCOS) kilichopo kata ya Ndugumbi, Wilaya ya Kinondoni , Mkoa wa Dar es salaam.
Ndugumbi Community Saccos kimesajiliwa kwa mujibu wa Sheria za Ushirika ya mwaka 2003 na namba yake ya usajili ni DSR 924 tarehe 10/11/2006.
NAMNA YA KUFIKA OFISI YA NDUGUMBI SACCOS COMMUNITY SACCOS
Eneo iliyopo ofisi hiyo inatazamana na Mwembe Chai Petrol Station ya Super Star
SIFA ZA KUWA MWANACHAMA WA NDUGUMBI COMMUNITY SACCOS
Kila chama cha Ushirika hapa nchini kina misingi na utaratibu wake wa kujiunga, na hizi sifa ni kwa mujibu wa sheria na katiba waliojiwekea katika kuongoza taasisi hiyo ili kuhakikisha wanafikia lengo
1;Awe na akili timamu
2:Awe tayari
3:Awe na na umri zaidi ya miaka 18
JINSI YA KUWA MWANACHAMA
Zifuatazo ni sifa za kuweza kupata na kujiunga na Ndugumbi Community Saccos
1: Lazima mwanachama alete picha za passporsize
2:Kiingilio Tsh.30000/=
3.Tsh 10000/=
4.Hisa moja Tsh20000/=
NB:Bila ya kuwa na hisa huwezi kuwa mwanachama, Pia ili uweze kuwa mwanachama lazima uwe na hisa zisizopungua 10.
TARATIBU ZA UWEKAJI
Mwanachama anaweza kuweka Akiba isiyopungua Tsh.10000/= kila mwezi
AKIBA ndio itakayomfanya mwanachama aweze kukopa si zaidi ya mara tatu.
AMANA ni pesa ambayo mwanachama anaweza kuchukua wakati wowote akihitaji.
Licha ya kutoa huduma hizo zote, lakini kila taasisi au vyama vya Ushirika havijapishana sana katika maswala ya mikopo
AINA ZA MIKOPO
1;Mkopo wa Maendeleo
Mkopo wa maendeleo ni mkopo unaotolewa kwa mwanachama ili aweze kujiendeleza kibiashara na atarejesha mkopo huo ndani ya muda uliopangwa
2;Mkopo wa Dharura
Mkopo wa Dharura ni aina ya mkopo uliokatika mfumo mzima wa Ndugumbi Community Saccos, mkopo huu hutolewa kwa mwanachama awe ana mkopo wa maendeleo au hana mkopo huo. Isipokuwa mkopo huu kurejeshwa ndani ya muda wa mwezi mmoja.
3:Mkopo wa Elimu
Mkopo huu wa Elimu na hutolewa kwa mwanachama ambaye anataka kusoma au ana mtoto/ndugu anayesoma atarejesha ndani ya muda wake wa masomo.
4;Mkopo wa NSSF
Mkopo huu nao ni kama aina nyingine ya mikopo iliyotangulia kuorodheshwa lakini mkopo huu hutolewa kwa mwanachama ambae ni mwanachama wa NSSF muda wa mkopo huu ni miaka miwili hadi mitano.
WAJIBU WA MWANACHAMA
Kwa kawaida wakati vyama hivi vinakwenda kuanzishwa tayari kulishakuwa na taratibu, kanuni na sheria ambazo zilipitishwa moja kwa moja kwa wanachama wake wanaotaka kujiunga na chama husika, moja ya wajibu huo ni kukubaliana kuwa chama kitakuwa na wajibu wa mwanachama wake lakini licha ya chama kuwa na wajibu wa mwanachama wake pia mwanchama ana wajibu kwa chama chake.
Ili uweze kuwa hai na kuendandana na uhalisia na mazingira ya Ndugumbi Community Saccos waliojiwekea kikanuni na kikatiba, ufuatao ni wajibu wa mwanachama;
1:Kuweka akiba mara kwa mara
2:Kukopa kwa mujibu wa masharti na sera za Saccos
3:Kurejesha mkopo kwa muda uliopangwa pamoja na
4:Kununua hisa za Saccos
Kauli mbio " KOPA KWA BUSARA-LIPA KWA WAKATI SACCOS KWA MAENDELEO"
Mwandishi wa makala hii ni Yusuph Mwamba +25557636650
Kwa mawasiliano zaidi wasiliana nasi kwa simu hapo chini
NDUGUMBI COMMUNITY SAVINGS AND CREDIT CO-OPERATIVE SOCIETY LTD
NDUGUMBI KINONDONI
S.L.P. 90269
SIMU:022172458
MOB:0715379379
0714369018
DAR ES SALAAM TANZANIA
IRINGA BRANCH
SIMU:026-2700455
Email:ndugumbisacoos@gmail.com
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment