Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba

CHAMA cha ushirika huu kilisajiliwa rasmi tarehe 23 Agosti 1968 na Msajili wa  Vyama vya Ushirika Tanzania kwa kupata hati ya usajili nambari CR 1861. Eneo la shughuli za chama hiki zipo katika eneo la Bandari ya Dar es salaam. (ndani ya shed Na.6 Annex).
MAONO (VISION)
Kuwa miongoni mwa Saccos inayoongoza kwa utoaji wa huduma bora za fedha Tanznia na Afrika kwa ujumla.

LENGO KUU  (MISSION)  
(a) Kupokea na kuweka akiba ya fedha za wanachama wake kwa faida, na kutoa mikopo ya masharti nafuu kwa wanachama wake.
(b)Kukuza akiba ya fedha ya wanachama kwa:
(1) Kuwahimiza watu wasio wanachama kujiunga na chama
(2)Kuwahimiza wanachama kuongeza mafungu (hisa) mawekezo yao (akiba)
(3)Kuanzisha na kuendeleza shughuli zozote za kiuchumi kwa manufaa ya wanachama kama itakavyokubalika na mkutano mkuu na kudhinishwa na mrajisi wa vyama vya ushirika.
UANACHAMA


Mtu atakayejiunga awe ni mfanyakazi wa mamlaka ya Bandari ya Tanzania (TPA). Mamlaka ya Bandari imegawanyika katika bandari kubwa na ndogo nazo ni Dar es salaam, Mtwara, Tanga, Mwanza, Bukoba, Mafia, Kigoma, Kyela, Makao Makuu (HQ) na Bagamoyo.

TARATIBU ZA KUJIUNGA
Mwanachama atatakiwa kufanya yafuatayo;
(a)Kiingilio Tsh. 15000/=
(b)Kuchangia akiba kuanzia Shs. 70000/=
(c)Kuchangia hisa ishirini ambapo thamani ya hisa ni shs. 10000/= na kufanya jumla ya shs 200000/=
(d)Malipo ya Michango hii itafanyika kwa njia ya "payroll" ya mshahara kwa kuwa hiki ni chama kiko eneo la kazi.
(e)Pindi mwanachama atakapokatwa kwa mara ya kwanza ndio atakuwa amejiunga na chama, hivyo kutatakiwa kuleta picha mbili za pasipoti kwa ajili ya reja na kitabu
(f)Pindi mwanachama akifikisha miezi mitatu atakuwa na haki ya kupata mkopo ili imradi anakatwa mchango wake kutoka kwenye mshahara wake na rejesho la mkopo halitaathiri 1/3 ya mshahara wake.


HAKI NA WAJIBU WA MWANACHAMA
(a)kuhakiki nyaraka zote za chama katika muda muafaka wa ofisi
(b)Kuchagua au kuchaguliwa kwenye uongozi
(c)Kutoa maoni binafsi kwa maendeleo ya chama
(d)Kupata riba itokanayo na akiba, hisa ndani ya chama


WAJIBU WA MWANACHAMA
(a)Kuweka akiba mara kwa mara 
(b)Kulipa madeni ya mkopo uliodhamini endapo mkopaji atashindwa kulipa 
(c)Kulipa mkopo uliodhamini endapo mkopaji atashindwa kulipa
(d)Kuhudhuria mikutano yote ya kikatiba

WANACHAMA 
(a) Wanachama kwa Umoja wao ndio wenye Mamlaka makubwa juu ya hatma ya chama
(b)Viongozi huendesha chama kwa mujibu wa maazimio ya Mkutano mkuu, Katiba, sheria kanuni na masharti ya vyama vya ushirika.

WAJUMBE WA KAMATI 
Kamati ya Usimamizi ina wajumbe watatu kamati ya mikopo, ina wajumbe watatu, wanaotokana na bodi
Bodi ina wajumbe watano mwakilishi wa chama


AINA ZA MIKOPO 
Aina za mikopo inayotolewa na chama ni 
(a)mkopo wa maendeleo
(b)mkopo wa dharura
(c)mkopo wa shule
(d)mkopo wa viwanja kulingana na ukubwa (sqm2)
(e)mkopo wa ujenzi (ujenzi kufikia hatua ya boma)
MKOPO WA MAENDELEO 
Shs. 3000000 hadi 30000000, muda wa mkopo miezi 60
Ni mara tatu ya akiba yako
MKOPO WA DHARURA
500000/= Muda wa mkopo ni miezi 6. mkopo yote riba ni 1.75% kwa mwezi
MKOPO WA SHULE 
Shs.1000000/=muda wa mkopo ni miezi 12 
VYANZO VYA FEDHA
(a)Akiba na Hisa za wanachama wenyewe
(b)Mikopo ya nje kutoka taasisi za fedha 
MAREJESHO 
Mikopo yote itakatwa kupitia mishahara ya wakopaji isipokuwa kama mkopaji anataka kumaliza deni upesi utaenda CRDB Bank PLC kulipa deni lake na ataleta slip ya kenki kwenye chama ili aandikiwe risiti

UANGALIZI NA UDHIBITI WA FEDHA  
Chama kimechukua tahadhari ya kuwa na akaunti za kuhifadhi fedha benki, chama kimeajiri watendaji , mhasibu, wahasibu wasaidizi, karani 3 na mhudumu 1
Hesabu za chama zinakaguliwa kila mwaka na Shirika la ukaguzi (COASCO) chama kina ofisi nzuri yenye usalama wa kifedha.
MATARAJIO YA CHAMA
1:Kuongeza wanachama wapya ili chama kiwe na nguvu hadi kufikia hatua ya benki
2:Kuhimiza wanachama waliopo waongeze akiba na michango yao ili kukuza mtaji wa chama
MAFANIKIO 

Chama kwa sasa kinajiendesha kwa kutumia mtaji wa ndani (Hakuna mkopo kutoka taasisi ya nje)
Tumepata viwanja kwa ajili ya ujenzi wa ofisi na kitega uchumi 
Chama kinamiliki gari kwa ajili ya kazi za nje, kufuatilia miradi ya chama
Pia chama  kinamiliki Bajaji kwa ajili ya shughuri za ndani na karibu ya ofisi
Tumefanikiwa kuendesha shughuli za chama kwa kutumia mfumo (system)
WADAU WA USHIRIKA
Serikali kuu
Wizara ya Ushirika , kilimo, na chakula
Benki kuu ya Tanzania
Mrajisi wa v yama vya Ushirika
CRDB Bank PLC Ltd
COASCO
SCCULT
Manispaa ya Temeke
Chuo kikuu cha Ushirika na ustadi za biashara Moshi
Vyama Vingine vya SACCOS vya nje na Ndani ya Nchi

UJENZI WA OFISI NA KITEGA UCHUMI
Kiwanja kilichopo karibu na makao makuu ya Wilaya ya Temeke Dar es salaam, ambacho kimenunuliwa na Binadamu Saccos kwa ajili ya Ujenzi wa ofisi na kitega uchumi
RAMANI YA VIWANJA 
Bandari Saccos imenunua viwanja maeneo ya Mataya Block 'J" Bagamoyo, Vumilia Ukooni, Mwongozo huko Kigamboni, Mvuti kidole, Tundwi Songani na Kimbiji kwa ajili ya makazi bora ya Wanachama.
Pia wanachama wanajengewa nyumba kwa gharama nafuu

ELIMU KWA WANACHAMA NA VIONGOZI
Bandarini Saccos Ltd huandaa Semina mbalimbali kwa ajili ya kuwaelimisha wanachama na viongozi kuanzisha na kuendesha miradi yao.
MAHUSIANO NA TAASISI ZA NDANI NA NJE YA NCHI
Bandarini Saccos Ltd ina mahusiano mazuri na taasisi/ Saccos za ndani na nje ya nchi kwa ajili ya kubadilishana uzoefu wa uendeshaji wa shughuli za Saccos kwa weledi
Makala hii imeandikwa na mwandishi wa habari Yusuph Mwamba +22557636650
BANDARINI SACCOS LTD
REG. No. 181
P.O.BOX 50091, DSM
Tel: 022-2138590-Ext. 2651
0754273387/ 0713 418344

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.