KLABU ya Soka ya Azam FC, imelazimishwa sare ya mabao 2-2 dhidi ya klabu ya soka ya Ruvu Shooting katika moja ya mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara uliofanyika jana kwenye Uwanja wa Azam Complex, uliko Chamazi, Dar es Salaam.
Matokeo hayo yanaifanya Wana ramba ramba hao wa Jiji la Dar es salaam ifikishe jumla ya alama 11 baada ya kucheza jumla ya michezo saba, huku ikishinda michezo mitatu , pamoja na sare mbili na kufungwa michezo miwili
Ruvu Shooting mpaka sasa wamefikisha jumla ya alama tisa baada ya kucheza jumla ya michezo saba, huku ikifanikiwa kushinda jumla ya michezo miwili,wakipoteza michezo miwili na sare tatu.
Ruvu Shooting wao ndio walikuwa wa kwanza kupata bao la kuongoza kupitia mchezaji wao Fullyuzulu Maganga kunako dakika ya nane ya mchezo , kabla ya raia wa Kinyarwanda Jean Baptiste Mugiraneza kuisawazishia Azam FC bao kunako dakika ya 46 akimalizia kona ya Khamis Mcha ‘Vialli’.
Mchezo huo ulio kuwa na kasi zaidi huku kila timu ikiwa na matumaini ya kuibuka na ushindi ilichukua dakika ya 70 baada ya Khamis Mcha"Viali" kuipatia Azam FC bao la pili , kabla ya mkongwe na aliyekuwa kiungo machachari wa Simba SC ,Shaaban Kisiga ‘Malone’ kuisawazishia timu yake bao la pili kunako dakika ya 89 mchezo kabla ya Refalii kupiga kipyenga cha mwisho.
Katika hatua nyingine, michezo mbali mbali ya ligi kuu Vodacom ili endelea huku Klabu ya soka ya Mbeya City ikifanikiwa kuibuka na ushindiwa bao 1-0 dhidi ya Mwadui FC Uwanja wa Sokoine, Bao pekee la Mbea City lilipachikwa kimyani na mwanandinga wake Ditram Nchimbi, wakati huo Mbao FC imelazimishwa sare ya 0-0 na JKT Ruvu Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza,huku wanalizombe wa Maji Maji imeambulia kichapo nyumbani kwake kwa jumla ya mabao 2-0 dhidi ya Stand United mjini Songea.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment