Na Yusuph Mwamba
SACCOS kwa maana ya
kawaida hujumuisha maana nyingi kutokana na uhitaji na mahitaji ya watu wengi katika
kukwamuana kiuchumi. SACCOS kama nyenzo
ya kujikwamua kiuchumi pia imekuwa na taratibu zake za kujiunga na uhalali wa
SACCOS pia unataratibu zake za
kuendeshwa kwa mujibu wa sharia ya ushirika namba 20 ya mwaka 2003.
Kila mwanachama anayeingia katika mfumo huu wa kujikwamua
kiuchumi ni lazima aelewe wajibu wa SACCOS kwa mwanachama na wajibu wa
mwanachama kwa SACCOS hatimaye kufahamu ni wakati gani uanachama wake utakoma
na mwisho kabisa kufahamu majina ya wanachama pamoja na Wajumbe wa Bodi ya uanzilishi
wa SACCOS.
SACCOS ni ufupisho wa neon la kingereza lenye tafasiri ya
Kiswahili inayosomeka kuwa CHAMA CHA USHIRIKA CHA AKIBA NA MIKOPO.
Hapa tunaenda kuangalia uanzishwaji wa WAVUVI SACCOS, (WAVUVI SAVINGS AND CREDIT
CO-OPERATIVE SOCIETY LTD) Ni Chama cha
ushirika cha akiba na mikopo chenye Makao makuu yake yaliyopo eneo la TUANGOMA
KIGAMBONI wilaya ya Temeke Jijini Dar es salaam, anuani ya chama hichi kwa
mujibu wa sharia ni S.L.P. 21811-DAR ES SALAAM.
Wavuvi Saccos, kilifanikiwa kuanzishwa mnamo Tarehe 1, Juni,
Mwaka 2013, namba ya kuandikishwa ni DSR 1431, shughuli zake ni Wafanya
biashara pamoja na Wafanya kazi, pia fungamano lake haswa liliwalenga wakazi wa
Kigamboni na hatimaye kuwafikia wakazi wa Sandali, Wilayani Temeke ambapo kuna
tawi linalojihusisha na maswala ya Saccos.
Wavuvi Saccos ni chama cha ushirika cha akiba na mikopo
chenye jumla ya wanachama wapatao 20 waliomba maombiyao kihalali hatimaye
kupewa uanachama na kiongozi au mwenyekiti wa chama hicho ni MAGRETH .L. MWENDA
Madhumuni ya uanishwaji wa chama hiki ni pamoja na kutoa
huduma kwa wananchi ili waweze kukidhi mahitaji mbali mbali ya kijamii ya
kiuchumi na kuinua hali ya maisha yao.
Licha ya kuangalia uanzishwaji wa WAVUVI SACCOS, tuangalie
kwa upande wa TANZANIA KWANZA FOUNDATION, Hii ni SACCOS pia inayojihusisha na
maswala ya kujikomboa kwa wanachi kwa upande wa kuweka na kukopa.
TANZANIA KWANZA FOUNDATION, ni Chama cha akiba na mikopo na
kutoa huduma kwa wananchi ili waweze kukidhi mahitaji mabali mbali ya kijamii
ya kiuchumi na kuinua hali ya maisha ya wanachama husika.
Chama hiki kina mwasisi wake anyejulikana kwa jina la HIDAYA
SHABANI SHOMVI marufu kama Binti Shomvi huku akisaidiwa na katibu wake anayejulikana
kwa jina la HUSNA ABDALLAH, Makao makuu ya Tanzania kwanza Foundation yapo
Wilayani Temeke, kata ya Sandali eneo la
Maganga.
TANZANIA KWANZA FOUNDATION, licha ya kujihusisha na shughuli
za akiba na mikopo kwa wanachama pia inajihusisha na maswala ya ,mazingira, Afya, Madawa ya kulevya pamoja na Mazingira.
Dhumuni la uanzishwaji wa
Tanzania kwanza Foundation
(a)Kuwawezesha jamii kuboresha huduma ya maji na kujenga
vyoo bora vya jamii
(b)Kujenga uwezo wa jamii katika kujiwekea akiba na kubuni
miradi mbali mbali ya ujasiriamali kupitia utoaji wa elimu
(c)Kuhamasisha jamii katika uboreshaji makazi kwa kuanzisha
michakato ya makazi bora na kuishawishi Serikali na watu wengine juu ya
upatikanaji wa ardhi yenye gharama nafuu pamoja na miundo mbinu.
(d)Kuhamasisha jamii juu ya utunzaji wa mazingira katika
kila kaya/mtaa kwa mtaa kwa kutoa elimu na kusaidia nyenzo mbalimbali za
kufanyia usafi
(e)Kuviwezesha vituo mbalimbali vinavyojihusisha na utoaji wa elimu kama vile
shule katika masuala ya msingi kama madawaiti, vitabu na vifaa muhimu vya
kujifunzia
(f)Kuhamasisha na kushirikisha vijana na wanajamii wengine katika
harakati/ kampeni mbalimbali kwa mfano masuala ya afya kwa kushirikiana na
wadau wa afya kutoka (HIV/AIDs), malaria, kifua kiukuu (TB), chanjo mbalimbali,
uzazi salama, kutumia maji safi, kutunza misitu, kilimo pamoja na ufugaji wa
kisasa.
(g) Kuhamasisha
wanajamii wote kupunguza na kujiepusha na matumizi ya madawa ya kulevya au
mihadarati.
Mbali na SACCOS,
Tanzania kwanza Foundation, imekwenda mbali zaidi baada ya kijikita na
maswala ya ujasiriamali ambapo kwa vyama vingi vya Ushirika wa akiba na kukopa
hapa nchini ni nadra sana kujihusisha na maswala kama hayo kitu ambacho ni
mfano wa kuigwa kwa SACCOS nyingine hapa nchini.
Baadhi ya ujasiriamali wanaojihusisha nao Tanzania kwanza
Foundation ni pamoja na :
(a)Utengenezaji wa jiki
(b)Utengenezaji wa sabuni za mawingu
(c)Utengenezaji wa
Tiles cleaner
(d)Utengenezaji wa sabuni ya maji
(e)Utengenezaji wa shampoo ya nywele
(f)Utengenezaji wa mafuta ya mgando meupe
(g)Utengenezaji wa Lotion
(h)Utengenezaji wa mishumaa
(i)Utengenezaji wa unga bora wa lishe
(j)Utengenezaji wa sabuni ya mche ya kawaida
(k)Utengenezaji wa Protex
(l)Utengenezaji wa sabuni ya muarobaini
(m)Utengenezaji wa sabuni ya Alovera
TARATIBU NA SIFA ZA KUJIUNGA NA WAVUVI SACCOS
(a)
Awe mwenye umri wa miaka isiyopungua 18 akiwa na
umri chini ya miaka 18 shughuli zake ziendeshwe na mzazi wake au mlezi
(b)
Awe mwenye tabia nzuri na akili timamu
(c)
Awe raia wa Tanzania kwa kuzaliwa au
kuandikishwa na anayekubalika kwenye masharti haya
(d)
Awe amelipa kiingilio, hisa na kuweka akiba na
awe anashiriki shughuli za SACCOS
(e)
Awe tayari kufuata masharti ya SACCOS, kanuni za
sharia ya vyama vya ushirika Na.20 ya mwaka 2003 na marekebisho yake wakati
wote.
(f)
Awe ni mkazi wa sehemu ya eneo la shughuli za
SACCOS
DHAMANA YA MIKOPO WAVUVI SACCOS
(a)
SACCOS inaweza kukopa baada ya kupata idhini ya
Msajili wa vyama vya Ushirika na Mkutano mkuu
(b)
Kiasi kisichozidi robo (¼ ) ya jumla ya his
azote pamoja na akiba, amana, kwa uamuzi wa angalau robo tatu (¾) ya wajumbe wa
bodi.
(c)
Kiasi zaidi kinaweza kukopwa baada ya kupata
uamuzi wa wanachama kwenye Mkutano Mkuu ambao wataafiki pendekezo lililofanywa
na robo tatu (¾) ya wajumbe wa Bodi, lakini kiasi kitakachokopwa kisizidi nusu
ya rasilimali ya SACCOS.
(d)
Dhima ya mwanachama kwa ajili ya madeni ya
SACCOS haitazidi kiwango cha hisa zake ndani ya SACCOS
WAVUVI SACCOS kwa ujumla ina vipengele vingi ambavyo ni mtaji na faida
kwa wanachama wake pia mikopo yao ni rahisi sana na mashariti yake siyo magumu
sana.
Badhi ya sehemu ambazo zili orodheshwa kwa mujibu wa sharia na kanuni za
chama hiki ni pamoja na Maombi ya mwanachama, kuacha na kusimamishwa uanachama,
kuteua mrithi, haki na wajibu wa mwanachama, haki kwa mwanachama, wajibu wa
mwanachama, wajibu wa SACCOS, (kiingilio, hisa, akiba na amana), kuuza au
kuahamisha hisa, mikopo ya taasisis za fedha, vyanzo vya fedha, hesabu za
chama, mgao wa dhiada, taratibu za uwekeji akiba, taratibu za mikopo, mkutano
wa SACCOS, mkutano mkuu wa kawaida, mkutano mkuu maalum, kuitisha mkutano
mkuu, uongozi wa chama, kazi za wajumbe
wa bodi, uchaguzi wa wajumbe wa bodi, upigaji kura, kukoma kwa ujumbe wa bodi,
kamti ya mikopo, pamoja na kuvunjwa na kufutwa kwa SACCOS.
Kwa mawasiliano zaidi Wavuvi Saccos wasiliana nasi kupitia
CCM Sandali Branch
TEMEKE DAR ES SALAAM
P.O.BOX 21811, DAR ES SALAAM
Mob:+255719000041
+255785000041
Email:wavuvisaccos@gmail.com
Tanzania kwanza Foundation (TAKWAF)
Maganga Magorofani, Dar es salaam
Mob: +255714021022
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment