KATIKA kuelekea pambano la kukata na shoka baina ya watani wa jadi Simba na Yanga maarufu kama Kariakoo Derby, Serikali imekuja na mfumo mpya wa ki elektoniki ambapo imekemea na kuwataka wale wenye nia ovu ya kutaka kuhujumu mfumo huu waache kabisa vinginevyo watakiona cha mtema kuni.
Waziri wa Habari Sanaa Utamaduni na Michezo Nape Nnauye alisema hawatakuwa tayari kuona mfumo huo ukiingiliwa na watu wachache ambao ni maharamia wa michezo kwa ajili ya maslahi yao binafsi huku Serikali ikikosa mapato baada ya kuziba mianya hiyo.
Kwa mujibu wa Waziri Nape, mfumo huo ni wa kwaanza wa aina yake katika eneo lote la Afrika chini ya Jangwa la Sahara, na utasaidia kuvuna mapato ambayo huko nyuma yalikuwa yakiangukia katika mikono haramu na kusababisha wanufaika halali kuvuja jasho la bure
"Kwa gharama yoyote hakutakuwa tayari kuona watu wanahujumu mfumo huu na tukiwabaini tutawachukulia hatua kali bila kujali nyadhifa zao wala uwezo wao wa kifedha.Alisema Waziri Nape
Nape alisema pia kumekuwa na changamoto kubwa za upatikanaji wa tiketi hizo katika kituo mbali mbali lakini zinashughulikiwa na hakuna mtu yoyote atashindwa kuangalia mchezo huo kwa kukosa huduma
Mbali na changamoto hizo, lakini mfumo huo utapelekea na kuufanya mfumo huo wa Uwanja wa Taifa kuwa wa kiusalama zaidi huku majina, anuani pamoja na maeneo wnayoishi kutambulika zaidi na kuziba minyanya ya waharifu.
"Mfumo huu ni mpya ni mgeni hanchini kwetu lazima changamoto kama hizi zijitokeze kulinganisha na ukubwa wa mechi husika, mashabiki wote wanaotaka kwenda uwanjani watapata nafasi ya kufanya hivyo watoa huduma wamejipanga kuhakikisha kila mtu anaenda uwanjani," alisema Nape.
Aidha Waziri Nape ameitaka kampuni ya Selecom ambayo ndiyo inaratibu upatikanaji wa tiketi hizo kuongeza idadi ya watoa Huduma ili kupunguza misururu ya watu kwenye vituo.
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment