WAHENGA WASEMA RAHA YA NGOMA UICHEZE, hapa ndipo tunakuja kuona mabadiliko ya Mashetani wekundu wa Oldtrafford Manchester United baada ya ujio wa Meneja mpya wa klabu hiyo Jose Mourinho.
Jana klbu bingwa ndogo maarufu kama Europa ligi iliendelea kushika kasi huku, Manchester United ikifanikiwa kuibuka na ushindi hafifu wa bao 1-0 dhidi ya timu ya Zorya Luhansk kutoka nchini Ukraini
Matokeo hayo ni matokeo hafifu sana kutokana na ukubwa wa klabu ya United na wengi wameyabenza matokeo hayo na kutodai na kuridhishwa na kiwango kilichoonenyeshwa na Mashetani hao licha ya kuibuka na ushindi huo.

Ushindi huo umeiweka United katika nafasi nzuri baada ya kupoteza mchezo wa kwanza walioucheza na klabu ya Feyennord huko Rotterdam kwa kuambulia kipigo cha bao 1-0.
Bao la ushindi la United, liliwekwa kimyani na Nyota wa kimataifa wa Uswizi , Zlatan Ibarahimovic kwa njia ya kichwa (free eder) kunako dakika ya 69 ya mchezo kufuatia krosi safi ya beki wao Fuso Mensah, na krosi kudondokea kwa Zlatani na kiuandikia United bao la kuongoza na la ushindi.
Licha ya kupata matokeo hayo, kuna maeneo muhimu yaliyopelekea United kupata ushindi dhaifu, Miongoni mwa maeneo hayo ni kama yafuatayo;
KUTOKUA MAKINI KATIKA SAFU YA USHAMBULIAJI
Hili nali ni tatizo ambalo liliwapelekea United, kuibuka na ushindi finyu, ukiangalia mchezo uliopita wa ligi kuu ya Uingereza dhidi ya mabingwa watetezi wa ligi kuu msimu uliopita klabu ya soka ya Leicer City kwa kuibuka na ushindi wa jumla ya mabao 4-1, kasi ya ushambuliaji wa United kiukweli haiko sawa ukitofautisha na mchezo uliopita ambapo tuliona muungano wa Zlatan pamoja na wenzake ulikuwa moto wa kuotea mbali, ukimwangalia Wayne Rooney pamoja na Zlatan utagundua wakicheza pamoja nguvu inakuwa kubwa sana huku viungo vyao wakiwa makini katika kupitisha mipara.
KUKOSEKANA KWA HERERA
Ili timu icheze inahitaji viungo washambuliaji wenye umakini mkubwa sana wa kupenyeza mipira kwa washambuliaji wao. Kukosekana kwa Herera amabye alicheza katika mchezo uliopita inawezekana ndio chanzo cha United kupata finyu lakini inaweza ikawa ni janja ya Mourinho katika mchezo ujao wa jumatatu dhidi ya Stoke City. Marouane Fellaini amekuwa katika mipango mizuri na Mourinho lakini simzuri katika kupitisha mipira ya mwisho kuliko Herera anayeonekana kuwa fundi zaidi ingawaje hayupo katika mipanggo ya Jose Mourinho.
KUPUUZWA KWA MICHAEL CARRICK
Michael Carrick ni kiungo anayeweza kutawala mipira zaidi haswa akiwa ndani ya eneo lake ni mwepesi na ni mtu sahihi sana katika kuhakikisha mashambulizi yanakuwa kwa kasi na kuwafanya wapinzani kukosa nafasi ya kuchezea mipira . Carrick ni bora zaidi kuliko Fellaini katika majukumu yao ya kazi.
Carrick mwenye umri wa miaka 35, amefanikiwa kucheza mchezo mmoja tangia kumalizika kwa mchezo wa ufunguzi wa ligi maarufu kama Ngao ya jamii.
UDHAIFU WA MARCOS ROJO
Moja ya jambo ambalo Jose Mourinho amelifanya ni kitendo cha kutomrejesha beki wake wa kushoto Daley Blind, baada ya kukosekana kwa Luke Shaw, hata kama United walionekana kucheza mpira na kuutawala kwa kiasi kikubwa lakini kitendo cha kumpanga Rojo kilikuwa sio sahihi kwa upande wake baada ya kufanya wapinzani kuwa chochoro yake katika kupeleka mashambulizi.
KUREJESHWA KWA NIDHAMU YA MCHEZO
Ushindi walioupata United, sio kuhamasiha tu bali ni kitu mabacho United walikua na kiu ya muda mrefu sana chini ya Jose Mourinho , kutokana kuwa na kikosi kizuri na kipana zaidi tunatgemea michezo ijayo dhidi ya Liverpool na Stoke City makosa haya hayataweza kujirudia tena na kujenga heshima iliyotoweka kwa muda mrefu tangu kuondoka kwa aliyekuwa meneja wa klabu hiyo Sir Alex Furguson
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia websiteTweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline

Post a Comment