Na Yusuph Mwamba
KLABU ya soka ya Manchester United, imemaliza ubishi na minong'ono iliyokuwa ikisikika mingoni mwa midomo ya watu wengi baada ya kumtia kitanzini mwanandinga wa kimataifa wa Sweden na klabu ya PSG Zlatan Ibrahimovic leo makao makuu ya klabu hiyo , tayari kuwatumikia mashetani wekundu wa Jiji la London ndani ya Old Trafford
Zlatani akiwaaga mashabiki wa Sweden kwenye moja ya mchezo ya michuano ya kombe la Euro 2016 |
Zlatan mwenye umri wa miaka 34, amesaini kunako klabu ya Manchester United akiwa mchezaji huru baada ya mkataba wake kumalizika kunako klabu yake ya PSG ya Ufaransa.
Kadabra ndani ya Old Trafford |
Ujio wa Zlatan United, kunamfanya mwanandinga huyo kufanya kazi kwa mara ya pili na Meneja huyo wa kireno Jose Morinho, baada ya awali kufanya kazi wote kunako klabu ya Inter-Milan ya Italia kwenye ligi kuu ya Serie A.
Zlatan akiwa na Jose Morinho kipindi yupo klabu ya Inter-Milan |
Ibrahimovic, anakuwa mchezaji wa pili katika usajili wa meneja huyo baada ya ule wa awali alioufanya wa kumsajili mlinzi wa kimataifa wa Ivory Coast na aliyekuwa akikipiga kunako klabu ya Villareal ya Hispain Eric Bailly.
Zlatan, amefanikiwa kumaliza msimu nwa ligi kuu ya Ufaransa akiwa na klabu ya PSG, amefanikiwa kucheza jumla ya michezo 180 na kufumania nyavu mara 156 huku akiwa ametumikia klabu hiyo kwa vipindi vinne vya msimu tangu atue kunako klabu hiyo akitokea klabu ya Inter-Milan.
Zlatan Ibrahimovic akitambulishwa rasmi United |
Katika ligi alizowahi chezea, zikiwemo Itali, Spain, na Uholanzi amefunga jumla ya mabao 392 katika michezo 677 aliyocheza ndani ya vilabu hivyo.
Mwanandinga huyo wa Sweden, amestaafu kuchezea timu yake ya Taifa mwaka 2016 katika michuano ya fainali ya Euro 2016 baada ya kuambulia kichapo cha bao 1-0 mbele ya Ubelgij ndipo maamuzi ya Zlatan kustaafu yakafanyika.
Katika michezo ya mechi za kirafiki za kujiandaa na maandalizi ya msimu ujao, klabu ya Manchester United itampa nafasi Ibrahimovic dhidi ya timu ya soka ya Galatasray ya Uturuki kwenye mchezo unaotarajia kufanyika Julai 30, 2016 katika Mji wa Gothenburg.
Zlatan amechezea timu yake ya Taifa jumla ya michezo 116 na katika hiyo michezo amefanikiwa kuzifumania nyavu mara 62.
Kauli ya Meneja mpya wa United, Jose Morinho baada ya ujio wa Zlatan Old Trafford
"Hatuna haja ya kumtambulisha Zlatan, historia yake na jina lake inataosha kumtambua , kwangu mimi ni mchezaji bora katika dunia hii ni mtu ninaye mkubali sana kwanza anakipaji cha hari ya juu na amekuja ligi bora duniani naamini atafanya kazi nzuri nilishawahi kuwa naye Inter-Milan namjua uwezo wake atarudisha heshima ya United iliyotoweka tangu kuondoka kwa aliyekuwa meneja wa zamani wa United, Sir Alex Furgason". Alisema Morinho
Post a Comment