Halloween party ideas 2015
Image

MSIYEMPENDA KAJA, WALES YAINGIA KATIKA HISTORIA  MPYA YA SOKA EURO 2016

Na Yusuph Mwamba

Huku mashindano ya fainali ya Euro 2016 yakiendelea kushika kasi katika hatua ya robo fainali, Timu ya Taifa ya Wales jana ilifanikiwa kuingia kwenye rekodi mpya ya soka kwenye michuano hiyo ya Euro 2016 baada ya kuiadhibu timu ya Taifa ya Ubelgij bila huruma kwa jumla ya mabao 3-1 katika mchezo uliochezwa kwenye Mji wa Lyon Ufaransa.

Ilichukua kunako dakika ya 13 ya mchezo, mwanadinga wa kimataifa na klabu ya AS Roma , Radja Nainggolan, kuipatia Ubelgij bao la kuongoza kabla ya mwanandinga, Ashley Williams anayekipiga kunako klabu ya soka ya Lile ya Ufaransa kuweza kusawazishia Wales bao kunako dakika ya 31 ya mchezo kuelekea mapumzikoni.
Hal Robson ,akishangilia goli lake pamoja na wachezaji wa timu ya Taifa ya Wales jana dhidi ya Ubelgij ambapo Wales walishinda 3-1

Timu zote zilionekana kucheza kwa kushambuliana, lakini timu ya Taifa ya Ubelgij ndiyo iliyokuwa ikitawala mchezo huo kwa asilimia kubwa kutokana na kujaza mastaa kama Eden Hazard anayekipaga klabu ya soka ya Chelsea, Thibot Countous Golikipa wa Chelsea, Romeu Lukaku pamoja na Batshuay hata hivyo majina hayawakusaidi wakijikuta wakiyaaga mashindano hayo ya Euro 2016 kwa adhabu ya magoli 3-1 dhidi ya taifa lenye nyota wachache wa kulipwa kama Gareth Bale anayekipiga klabu ya Real Madrid mabingwa wa Uefa 2016 huku wakichukua mara 11 tangu kuanzishwa kwake.
Joe Allen ,akimthibiti Eden Hzard wa Ubelgij  kwenye mchezo wa robo fainali ya Euro 2016 jana ambapo Wales walishinda 3-1 

Hadi timu hizo zinakwenda mapumziko zilikuwa zkitoshana nguvu ya bao 1-1

Dakika chache ya mchezo ya kipindi cha pili, Hal Robson Kanu aliweza kuiandikia Wales bao la pili kunako dakika ya 55, baada ya mwaanandinga ,Sam Vokes, kupigilia msumari wa mwisho na bao la ushindi la timu ya Taifa ya wales kunako dakika ya 86 ya mchezo kumalizika na kufanya hadi kipyenga cha mwisho cha mwamuzi kinalia matokeo kusomeka Wales 3-1 dhidi ya Ubelgij.
Sam Vokes ,akiwanyanyua mashabikiwa Wales baada ya kupigilia msumari wa mwisho na wa ushindi kwa timu ya Taifa ya Wales jana ambapo Wales wamefanikiwa kuingia hatua ya nusu fainali Euro 2016

Licha ya  Meneja wa Ubelgij, Chris Coleman, kufanya mabadiliko ya kuwatoa baadhi ya nyota wake kama Yannick Ferreira Currasco na nafasi yake kuchukuliwa na Maroune Fellaini, huku akimtoa nyota Jordan Lukaku na nafasi yake kuchukuliwa na Dries Mertens na kumtoa Romelu Lukaku na nafasi yake kuchukuliwa na Michy Batshuay lakini mabadiliko hayo hayakuweza kuzaa matunda.
Nahodha wa timu ya Taifa ya Wales, Ashley William akishangilia bao lake la pili dhidi ya Ubelgij jana 

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Wales ; Hennessey, Gunter, Williams, Chester, Davies, Taylor, Allen, Ramsey (J Collins, 90), Ledley (King, 77), Bale, Robson-Kanu (Vokes, 74).

Kikosi cha Timu ya Taifa ya Ubelgij ; Courtois, Meunier, Alderweireld, Denayer, J. Lukaku (Mertens, 75), Witsel, Nainggolan, Carrasco (Fellaini, 46), De Bruyne, Hazard, R. Lukaku (Batshuayi, 83).

Kwa matokeo hayo, timu ya Taifa ya Wales, itaumana na timu ya Taifa ya Ureno kwenye mchezo wa nusu fainali ya michuno ya Euro 2016 inayotarajia kupigwa  Julai 6, 2016 siku ya Jumatano.

 Mchezaji bora wa mchezo alikuwa  Aaron Ramsey

Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.