Na Yusuph Mwamba
KLABU ya soka ya Everton na klabu ya Soka ya Napoli zimeingia katika vita ya kuwania saini ya mwanandinga wa kimataifa wa Ubelgij na klabu ya Zenet St Petersburg ,Axel Witsel, baada ya vilabu hivyo kuonesha nia ya kumtaka nyota huyo.
Axel Witsel ,akitafuta mbinu ya kumtoka adui |
Witsel mwenye umri wa miaka 27, amekuwa akiwaniwa na vilabu hivyo kutokana na kuvitiwa na kiwango chake alichokionesha kwenye ligi yao msimu uliomalizika na kwenye michuano ya fainali ya Euro 2016 inayoendelea kutimua vumbi Nchini Ufaransa.
Mwanandinga huyo, alianza kucheza kwenye ligi yao ya nyumbani akiwa na umri wa miaka 19 na kuamua kutimkia kunako klabu ya Benifica ya Ureno mwaka 2011-2012
Axel Witsel , akiwanyooshea mikono ikiwa ni ishara ya mashabiki wa timu yake washangilie katika moja ya mchezo akiwa Zenet St Petersburg ya Urusi |
Mwaka 2012 alisaini kunako klabu ya soka ya Zenet St Petersburg kwa dili la pauni milioni 34 kwa kandarasi ya miaka mitano ambapo alikuwa chini ya Meneja Andrew Villas Boas
"Nimekutana na mkurugenzi wa timu ya Napoli, Christiano Giuntol, lakini mmi ni mchezaji ambaye najua ninachokifanya nitacheza popote ili mradi pawepo na maslahi, soka ni ajira na pia klabu ya Napoli ni klabu kubwa sana licha ya everton kuonesha nia ya kunihitaji lakini kikubwa ni makubaliano baina ya timu zote na endapo makubaliano yatakwenda vizuri nitajiunga na timu itakayo kubaliyana na mimi"
Witsel akiwa na timu ya Taifa ya Ubelgij kwenye michuano ya fainali ya Euro 2016 Nchini Ufaransa |
Post a Comment