Na Yusuph Mwamba
KLABU ya soka ya West Ham United imekamilisha dili la kumsajili winga wa kimataifa wa Uturuki ,Gokhan Tore, kwa ajili ya kuitumikia klabu hiyo katika msimu ujao wa ligi kuu Uingereza maarufu kama EPL Premier League.

Usajili wa mwanandinga huyo umefanikiwa kuigharimu klabu ya soka ya West Ham United kiasi cha pauni milioni 2.5 ikiwa ni ada kwa ajili ya mkopo kutoka klabu ya soka ya Besiktas lakini pia kutampa uhuru mwanandinga huyo kama atakubali kusaini moja kwa moja kunako klabu hiyo mwisho wa msimu baada ya mkopo kumalizika
Licha ya kupambana sana, lakini Tore hakuweza kufanikiwa kipindi akiitumikia klabu yake ya Rubin Kazan ya Nchini Russia kabla ya kujiunga na Besiktas.
Hatua ya kumtoa mwanandinga huyo kwa mkopo ilianzia msimu wa mwaka 2013-14 hatimaye na kupata kuwa mchezaji wa kudumu mnamo msimu wa mwaka 2014.
Hata hivyo, alifanikiwa kumaliza msimu wa ligi 2015/2016 akifanikiwa kutikisa nyavu mara 19 katika michezo 111 aliyocheza akiwa na timu yake ya Besiktas lakini hakufanikiwa kuorodheshwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Uturuki kilichokuwepo kwenye fainali ya michuano ya kombe la Euro 2016 Nchini Ufaransa.
" Nafurahi sana kutua West Ham, nilikuwa nikifuatilia baadhi ya michezo yao na ndio kitu ambacho kilinivutia kujiunga na klabu hii". Alisema Tore
"Utumwa umenifanya nijiunge na klabu hii, na ndio sababu kubwa iliyopelekea kuwa hapa West Ham, kocha wao ni mtu mwenye msaada sana na mimi na mjua vizuri naye ananijua tarajieni kazi nzuri kutoka kwangu kikubwa ushirikiano ni kocha mzuri sana ni kama baba yangu na hapa ni kama familia yangu " Aliongeza Tore
JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia, bila ya kuingia website
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline
Post a Comment