Halloween party ideas 2015
Image

 Na Yusuph Mwamba

MENEJA mpya wa klabu ya soka ya Manchester United, Jose Mourinho, ameanza harakati za kuitengeneza timu baada ya kuomba hamasa kwa mashabiki wa klabu hiyo katika kudumisha umoja na mshikamano ili timu iweze kufanya vizuri msimu ujao wa ligi kuu na mashindano mbalimbali
Kocha wa United Jose Mourinho



Mourinho ambaye alikuwa meneja wa zamani wa klabu ya soka ya Chelsea FC, kabla ya kujiunga na mabingwa wa kombe la Uefa mara 11 na matajiri wa soka Duniani klabu ya Real Madrid ameanza tambo za kujihami na kuwataka washabiki wa klabu hiyo watoe ushirikiano ili kuhakikisha timu inafikia malengo yake.
Zlatan Ibrahimovic

"Huu ni mwanzo mzuri kwangu kuhamasisha washabiki wabgu . unajua swala la ushindi huchangiwa na mshikamano wa washabiki kwahiyo kama hatutakuwa wamoja na kutokuwa na mshikamano sidhani kama matokeo yatapatikana, pia timu ikiharibu huwezi kusema kusema wachezaji wapya wameharibu, wala kocha kaharibu pale itabakia kuwa Manchester United ndiyo imeharibu kwahiyo nawaombeni sana ushirikiano wenu ".Alisema Mourinho
Henrikh Mkhitaryan

Pia aliongeza kuwa "  swala lakuja kwangu United ni kupata matokeo mazuri na kuifikisha timu katika hatua nzuri ya kimaendeleo ya soka kwahiyo mtarajie ushindi na makombe japo haitakuwa kazi rahisi kwa vile tunao washindani wetu lakini kama mtanipa ushirikiano wa kutosha naimani mambo yatakuwa mepesi na kurudisha heshima iliyopotea muda mrefu tangu aondoke Sir Alex Farguson"


Mpaka sasa klabu ya Manchester United imewasajili Nyota watatu akiwemo Zlatan  Ibrahim Movic,Henrikh Mkhitaryan, pamoja na  Eric Bailly
Eric Bailly


JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia website

Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline







Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.