Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba

Mwanandinga wa kimataifa wa Uhulanzi na klabu ya soka AZ Aikmaar, Vincent Janssen, yupo mbioni kumwaga wino kunako klabu ya soka ya Totenham Spurs tayari kuitumikia klabu hiyo yenye maskani yake White Heart Jijini London
Janssen Vicent

Vincent, aliyefanikiwa kumaliza ligi kuu ya Uholanzi msimu wa mwaka 2015/2016 ,amefanikiwa kuweka kimyani  jumla ya magoli 27 na kuwa miongoni mwa wafungaji bora watano katika ligi yao  msimu uliopita, amekubali kusaini dili la pauni milioni 18.8. kama ada ya uhamisho wa mwanandinga huyo.

Janssen, mwenye umri wa miaka 22 ,aliyejiunga na klabu ya soka ya AZ Aikmaar akitokea klabu ya Almere City 2015 , alikuwa akiwaniwa na baadhi ya vilabu vikubwa duniani ikiwemo Paris Saint Germany (PSG) , halikadhalika na klabu ya Wolfsburg ya Ujerumani ambapo vyote vilimtaka kwa pauni milioni 15 lakini dili lake likaangukia kunako klabu ya Spurs.


Kocha mkuu wa Spurs,Mauricio Pochettino, na akishirikiana na msaidizi wake Jesus Perez pamoja na mkurugenzi wa ufundi wa klabu ya Spurs walikuwa wakimfuatilia mwanandinga huyo tangu kuanza kwa harakati za kutafuta mshindi kwenye makundi ya kuwania kushiriki fainali ya michuano ya kombe la Euro 2016 ambapo Uholanzi ilipokutana na Timu ya Taifa ya Jamhuri ya Ireland .
Janssen Vicent


JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia website

Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline






















Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.