Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwama

KLABU  ya soka ya Real Madrid, imejitoa rasmi kwenye kinyang'anyiro cha kuwania saini ya uhamisho wa mwanandinga wa Kimataifa wa Ufaransa ,Paul Pogba, baada ya kushindwana kibiashara na mwanandinga huyo.
 
Uhamisho wa Pogba ,unatarajia kugharimu kiasi cha pauni milion 85, ukilinganisha na usajili mzima wa kiungo huyo , ikiwa pamoja na bonusi ya mchezaji huyo pamoja na wakala wake kwahiyo jumla ya uhamisho wake utagharimu kiasi cha pauni milioni 123.
Paul Pogba

Uamuzi huo wa Real Madrid,umefikiwa baadaya chanzo kutoka kunako klabu hiyo kusema kuwa sababu kubwa ya kujitoa kuwania saini ya mwanandinga huyo ni sababu za kibiashara juu ya uhamisho wake ikisemekana dau la mwanandinga huyo kuwa kubwa mno .

Licha ya klabu hizo kutofikia maamuzi lakini bado wakala wa mwanandinga huyo, Mino Raiola, amezidi kuwa karibu sana na Madrid ili kutaka klabu hiyo kumchukua mwanandinga  japo dili hilo limeonekana kuota mbawa.

Klabu ya Man United, imeonekana kuwa na nia ya kumnyakua mchezaji huyo, lakini tusubirie wiki moja iliyobaki kabla ya pazia la usajili kufungwa ,lakini Rais wa Real Florentino Perez amesema pesa wanayohitaji ni kubwa sana.

Endapo mwanandinga huyo atakubali kusaini kunako klabu ya Man United, basi mshahara wake utagharimu kiasi cha milioni 250000 kwa wiki huku akiwa ndani ya kandarasi ya miaka mitano .
Pogba akijaribu kuwatoka walinzi wa Ac Milani katika moja ya mchezo wa ligi SerieA


Pia kiungo wa kimataifa wa timu ya Taifa ya Italia, Alessando Del Piero, amesema angependa kumuona Pogba ,akitumikia Turini kunako klabu ya Juventus msimu ujao na kusema hapo ndipo mahala sahihi palipo mpa mafanikio tangu ajiunge na klabu hiyo akitoke Man United akiwa mchezaji huru kwa kile kilichosemwa na aliyekuwa meneja wa zamani wa klabu ya United Sir Alex Furgason kutokuwa na nidhamu katika timu.
Piro akipongezana na Pogba



Wakati huo, dili la Pogba likionekana kuwa kikwazo, Real Madrid wamegeukia upande wa mwanandinga na kiungo wa Kimataifa wa Ureni na kunako klabu ya soka ya Valencia, Andrew Gomes, kutua kunako klabu hiyo.
Andre Gomes

Gomes, anatarajia kutua kunako klabu hiyo, kwa dau la Euro 42 sawa na pauni milion 50 baada ya makubaliano ya awali  yaliyofikiwa baada ya kumalizika kwa fainali ya michuano ya Euro 2016 Nchini Ufaransa na Ureno kufanikiwa kunyakuwa taji hilo.

JIUNGE NASI , BONYEZA HAPA http://www.wabunifumedia.blogspot.com ku-install App ya wabunifumedia,  bila ya kuingia website

Tweet@wabunifumediaonline, youtube@wabunifumediaonline TV, Fb@wabunifumediaonline, insta@wabunifumediaonline









Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.