TAMSHA LA ZIFF LAMUENZI BI KIDUDE.
Na Yusuph Mwamba
MILANGO yaTamasha la Kimataifa la Filamu za Nchi za Jahazi (ZIFF) ambalo linafanyika kwa mara ya 19 imewekwa wazi siku ya leo na kuandika historia kubwa kwenye suala la kukuza na kuuendeleza utamaduni wa mwafrika baada ya waandalizi hao wakiwa nania ya kutaka kumuenzi Hayati Bibi Kidude
Kwa kutambua mchango wa Wasanii Nguli wa muziki asilia hapa Nchini, Tamasha la Kimataifa la Filamu za Nchi za Jahazi (ZIFF) ambalo kwa mwaka huu linatimiza miaka 19 tangu kuanzishwa kwake lengo kubwa likiwa ni kukuza na kuendeleza utamaduni wa Mwafrika kupitia maonyesho ya filamu, muziki na sanaa mbalimbali.
Tamasha hili limeanza rasmi jana huko Visiwani Zanzibar ambapo tamati yake ni Julai 17, limefanikiwa kuwaleta karibu watu wa mataifa mbalimbali kupitia kauli mbiu ya "Ndiyo hii Safari Yetu", ambapo Marehemu Bi. kidude alienziwa kupitia sanaa ya uimbaji.
Baby J, alitumia dakika kadhaa jukwaani kuperfom nyimbo za gwiji la muziki asilia visiwani humo ,Bi.Kidude, ambaye kwa sasa ni marehemu.
![]() |
Nguli wa filamu kutoka India Kunal Kapoor |
Post a Comment