Halloween party ideas 2015
Image

Na Yusuph Mwamba

KIKOSI cha timu ya Taifa ya Ubelgij kimefanikiwa kujiweka kwenye mazingira mazuri ya kutinga hatua ya 16 bora ya fainali ya michuano ya Euro 2016 baada ya kuwatelemshia kichapo kikali timu ya Taifa ya Jamhuri ya Ireland kwa jumla ya mabao 3-0.

Mabao ya Ubelgij yaiwekwa kimyani na Mwanandinga anayekipiga kunako klabu ya Everton Romeu Lukaku kunako dakika ya 48 punde baada ya vikosi hivyo kurejea dimbani.

Kipindi cha kwanza, timu zote zilionekana kushambuliana kwa kasi, huku Ubelgij inayoongozwa na nyota wa Kimataifa na Klabu ya Chelsea Eden Hazard pamoja na mlinda mlango wa timu hiyo Courtois ikionekana kutawala mchezo huo kwa asilimia kubwa licha ya kipindi cha kwanza kutoshana nguvu ya 0-0.

Kocha wa Ubelgij, kipindi cha pili alifanya mabadiliko na kuwatoa baadhi ya nyota wake Carrasco na Dembele na nafasi zao zikachukuliwa na wanandinga Mertens aliyechukua nafasi ya Carrsco huku Nainggolan akichukua nafasi ya Dembele aliyepata majeraha ya mguu.

Mabadiliko hayo yalionekana kuzaa matunda, kwani kunako dakika ya 61 mwanandinga Witsel alifanikiwa kuwaamsha mashabiki wa Ubelgij kwa goli safi na kufanya matokeo kusomeka 2-0, hata hivyo Ubelgij waliendelea kulisakama lango la Ireland na kunako dakika ya 70 ya mchezo Lukaku tena akafanikiwa kupigilia msumari wa mwisho na wa ushindi wa timu hiyo, hadi kipyenga cha mwamuzi kinapulizwa matokeo yalisomeka Ubelgij 3-0 Ireland.

Kwa matokeo hayo, Jamhuri ya Ireland wanahitajika kufanya kazi za ziada ili kuibuka na ushindi dhidi ya timu ya Taifa ya Italia Juni 22,2016 ya wiki ijayo kama itahitaji kusonga mbele, pambano jingine litakuwa kati ya timu ya Taifa ya Sweden dhidi ya Ubelgij ambayo inahitaji alama chache kujihakikishia kufuzu 16 bora huku Italia ikiwa tayari imefanikiwa kufuzu hatua hiyo.

Kikosi cha Ubelgij; Courtois, Meunier, Witsel, Alderweireld, Dembele, Vermaelen, Vertonghen, Ferrera carra, Debruyne, Eden Hazzard, Romeu Lukaku na mfumo waliotumia ni 4-2-3-1.

Kikosi cha Jamhuri ya Ireland; Randolph, Coleman, O"shea, Clark, Ward,Handrick, Whelan, Mc carthy, Hoolahan, Long na umfumo waliotumia ni 4-4-1-1

Kundi F, linaongozwa na Italia yenye jumla ya alama 6 ikifutiwa na timu ya Taifa ya Ubelgij yenye alama 3 huku Sweden na Jamhuri ya Ireland kila mmoja akiwa na alama moja moja.



Witsel akipongezana na Lukaku baada ya kuiandikia Ubelgij bao la pili 









Lukaku akishangilia bao lake la pili kwenye mchezo dhidi ya Ireland  leo





Mlinziwa Ubelgij akijaribu kuokoa hatari langoni mwake dhidi ya Ireland 









Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.