Na Mwandishi wetu.
KIUNGO wa Mbeya City FC , Ramadhani Chombo ‘Rendondo’ ameionya timu ya Yanga kuwa ijiandae vya kutosha itakapokwenda jijini Mbeya mwanzoni mwa juma lijalo kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kati ya timu hizo mbili uliopangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Sokoine, Mei 10 mwaka huu.
KIUNGO wa Mbeya City FC , Ramadhani Chombo ‘Rendondo’ ameionya timu ya Yanga kuwa ijiandae vya kutosha itakapokwenda jijini Mbeya mwanzoni mwa juma lijalo kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu ya Vodacom Tanzania bara kati ya timu hizo mbili uliopangwa kuchezwa kwenye uwanja wa Sokoine, Mei 10 mwaka huu.
Akizungumza na mbeyacityfc.com, Redondo aliyekosa michezo miwili ya awali kupisha majeraha ya mguu kabla ya kurejea na kuichezea City kwenye mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar aliweka wazi kuwa ana imani kubwa na kikosi cha sasa cha timu yake, hasa baada ya ujio wa kocha Kinnah Phiri aliyefanikiwa kuyaondosha ‘makandokando’ yote yaliyokuwa yakisababisha timu kufanya vibaya kwenye michezo iliyopita.
“Nadhani Yanga wanatakiwa wajiandae vizuri, wanakuja kukutana na kikosi cha City ambacho kiko kwenye wakati mzuri hivi sasa, hivyo wasitegemee mteremko, ujio wa kocha Phiri umeiimarisha zaidi timu yetu, ametupa muongozo mzuri na amefanya kazi kubwa kuweka timu sawa, hivyo hao wanaokuja wajue watakutana na upinzani mkali, timu yetu sasa inacheza tofauti sana na ilivyokuwa inacheza hapo mwanzo”, alisema.
Akiendelea zaidi Redondo, aliyewahi kucheza kwa mafaniko kwenye timu za Ashanti, Simba na Azam Fc alisema kuwa anafahamu mchezo utakuwa mgumu pande zote kwa sababu kila timu inahitaji matokeo kulingana na hali ilivyo kwenye msimamo, Yanga ikitaka kujihakikishia ubingwa na City ikihitaji kujiweaka kwenye mazingira mazuri zaidi licha ya kuwepo kwa uhakika kuwa itasalia kwenye ligi .
Kuhusu majaaliwa yake kwenye kikosi cha City Redondo alisema kuwa anaimani kubwa atakuwa sehemu ya kikosi msimu ujao, na kuweka wazi furaha yake ya kuwa mchezaji wa timu hii tangu alipojiunga nayo mapema mwezi Januari.
“Nilijiunga na City mapema mwezi Januari, nakumbuka ilikuwa ni wakati wa usajili wa dirisha dogo, binafsi nina furaha hapa na nitaka kufanya kazi zaidi na kwa uwezo wangu wote kwa sababu lengo langu ni kuendelea kuwepo, kwangu mimi hii ni timu nzuri kuliko zote nilizowahi kucheza, kuna wakati najiuliza kwa nini sikuwa huku mapema lakini hii ni soka na maisha ya mchezo huu ndiyo yalivyo” alimaliza.
Post a Comment