Na Yusuph Mwamba
KIKOSI cha Yanga kikijiandaa na mchezo wao dhidi ya Mo Bejaia leo juni 19, Tayari benchi la ufundi wameanza mikakati ya kuwajadili nyota wake wapya Kessy na Mahadhi ambao majina yao yamewasilishwa katika shirikisho la soka la Afrika CAF kwa ajili ya kuthibitiosha kutumika kwao katika michuano hiyo. ilwasije kuingia mkenge.
Akizungumza na wanahabari, meneja wa klabu hiyo ambao ni mabingwa wa Tanzania bara na kombe la shirikisho Azam Federation Cup ,Hafidh Saleh, mapema leo amesema kwamba taarifa za wasiwasi juu ya kuwatumia wanandinga hao wamezipata asubuhi ya leo na kwamba wanajipanga kukutana kwa ajili ya kujadili swala hilo kabla ya kuelekea mchezoni.
Yanga ambao ni wawakilishi pekee kutoka ukanda wa afrika mashariki na kati katika michuano hiyo ya shirikisho barani afrika wanatupa karata yao leo jumapili juni 19, 2016 dhidi ya klabu hiyo ya Mo Bejaia ya Algeria ,mchezo utakaochezwa majira ya saa moja usiku kwa saa za huko sawa na saa tatu usiku kwa saa za hapa nyumbani.
Hassan Kessy akijiandaa na mazoezi |
Post a Comment