Na Yusuph Mwamba
MMILIKI wa klabu ya Soka ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Moise
Katumbi,amehukumiwa kwenda jela miaka mitatu.
Moise Katumbi |
Kufuwatia kuhukumiwa kwa Katumbi mika mitatu, kuna kwenda sambamba na kutozwa faini ya dola milioni 6 kwa kosa la kujimilikisha eneo.
Rais huyo wa TP Mazembe, pia alikuwa na dhamira ya kugombea nafasi ya Urais wa Kongo katika uchaguzi unaotarajia kufanyika mwisho wa mwaka 2016 kupita chama cha upinzani kushindana na Rais anayekaribia kumaliza muda wake kwa awamu ya sasa Rais Joseph Kabila.
Hata hivyo, wakati hukumu hiyo ikitolewa,Moise Katumbi, alikuwa hayupo Nchini Congo, alikuwa akasafiri kuelekea Afrika Kusini kupata matibabu.
Baadhi ya makosa mengine yaliyompelekea Katumbi kuhukumiwa jela , ni pamoja na swala la kuajiri wa geni kutoka nje ya Kongo kwa ajili ya kuandaa njama za kumuondoa
Rais Kabila katika kinyang`anyiro cha kugombea Urais wa Nchi hiyo..
Moise Katumbi akisalimiana na wachezaji wake |
Miongoni mwa mafaniko aliyoyapata Moise Katumbi ni pamoja na kuwa Rais wa kwanza wa klabu ya TP Mazembe aliyeiongoza klabu hiyo kucheza hatua ya fainali ya klabu bingwa ya Dunia dhidi ya klabu ya Inter Milan desemba 18, 2010 ,ikiwa chini ya Jose Morinho, rekodi ambayo imeifanya TP Mazemba kuwa klabu pekee Barani Afrika kufikia hatua hiyo, na sasa Mazembe wanakuja Tanzania kucheza mchezo wao wa pili wa nane bora dhidi ya Yanga, mchezo utakao pigwa juni 29, 2016 kwenye Uwanja wa Taifa Dar Es saalam majira ya saa moja usiku.
Wachezaji wa TP Mazembe wakishangilia goli katika moja ya mchezo wao |
Katumbi akiwa kwenye mahojiano maalumu na waandishi wa habari |
Post a Comment