POLISI mkoa wa Ilala inamshikilia mtuhumiwa mmoja kwa kosa la utapeli na kutumia vibaya jina la Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda.
Akizungumza na waandishi wa habari , Kamanda wa Polisi Mkoa wa Ilala, Salum Hamduni alisema wamefanikiwa kumkamata kijana mmoja anayejulikana kwa jina la Imarock Rutashobya (37) mkazi wa Pugu kwa tuhuma za kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu wa kutumia jina la mkuu wa mkoa Paul Makonda.
Kitendo hicho kilitokea juni 16, mwaka huu.Alisema baada ya mtuhumiwa huyo kudiliki kumpigia simu Mkurugenzi wa kampuni ya Jones Logistic Ltd, James Lupondo na kujitambulisha kwa mtu huyo kuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kwa lengo la kumsaidia kijana ambaye amepata ufadhili kwenda kusoma nje ya Nchi.
Mtuhumiwa huyo alidai Lupondo achangie asilimia 30 sawa na dola za Kimarekani 3,500 ya gharama za chuo kilichopo nchini Ufilipino, baada ya kupata ufadhili wa asilimia 70.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Poul Makonda, akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake jana juu ya wale wanaotumia jina lake kufanya utapeli wa kujipatia fedha kinyume na sheria na kanuni za Nchi
Aliongeza kuwa, katika maongezi yake baina ya kijana huyo na Lupono , mtuhumiwa huyo alimweleza Lupondo kuwa kuna namna tofauti za kutuma fedha hizo za msaada, ikiwa ni pamoja na kuweka kwenye akaunti ya benki au kutoa fedha taslimu huku akimtajia namba ya simu ya kijana anayehitaji msaada huo ambayo ni 0717 338473 na kusema huyo kijana atafika ofisini kwake baada ya saa mbili akiwa na nyaraka zote za fursa ya hayo masomo.
“Naomba nitoe rai na onyo kwa wale wote wenye tabia mbovu kama hizi za ya kutumia majina ya viongozi wa Serikali kwa ajili ya kujipatia kipato ife mara moja na endapo utagundulika hatua kali nza sheria zitafuta juu yako na kusisi tiza wanachi wanatakiwa kuwa makiniwanapopigiwa simu na watu wasiowafahamu na kujitambulisha kwao kwa majina ya viongozi” Alisema Hamduni.
Alisema licha ya kutumika kwa jina la Makonda, pia wapo baadhi ya watu wengine wenye michezo michafu wamekuwa wakitumia majina ya viongozi wa Serikali ikiwemo jina la Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kuwatapeli watu wenye fedha.
Post a Comment