Halloween party ideas 2015
Image

KITENDO CHA KIGOGO KUPORA ARDHI YA HEKALI 2000 CHA ZIDI  KUWATESA WAKAZI WA MVUMI WILAYANI KILOSA, MOROGORO

Na Yusuph Mwamba

Rais Magufuli, amekuwa akichukua hatua mbalimbali dhidi ya mtu watu au taasisi na kuwaita majipu,moja ya hatua hizo ni kutengua uteuzi na kupisha uchunguzi kama ilivyokuwa kwa aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Anna Kilango baada kutoa Takwimu isiyo sahihi kuhusu wafanyakazi hewa.

Rais pia amekuwa akitumbua majipu mbali ikiwemoTCRA,BOT,NIDA,TRL,Muhimbili na maeneo mbalimbali kwa lengo la kulinda maslahi ya wananchi na taifa kwa ujumla
Serikali yoyote Duniani ipo kwa ajili ya ustawi wa wananchi, hivyo wananchi wa Kijiji cha Mvumi Kata ya Mvumi wilaya ya Kilosa wameamua kuangusha kilio chao kwa Rais Magufuli baada ya kutotendewa haki na Muwekezaji waliye mtaja kwa jina la, Jitu Pateli, ambaye wanadai amewapora maeneo yao ya ardhi na kujimilikisha huku akitoa vitisho kwa watu watakao tumia maeneo hayo na wanadai amekuwa akishirikiana na vyombo vya Dola kuwakamata wakazi hao na kuwafugulia mashtaka kunyume na utaratibu

Mwenyekiti wa kijiji cha Mvumi, kata ya Mvumi, wilaya Kilosa Mkoa wa Morogoro, Abdully Tumbo akifafanua juu y sakata la kigogo kupora ardhi ya hekali 2000 na kuwanyanyasa wanakijiji hao kinyume na sheria za Nchi
Akiendelea kufafanua kadhia hiyo, Mwenyekiti wa Kijiji hicho, Abduly Tumbo, amesema kuwa mwekezaji huy amewapora ardhi Wanakijiji ambapo yeye kihalali anamiliki jumla ya hekali 520, lakini cha kushangaza anadiliki kumiliki zaidi ya hekali 2000 huku akitumia hekali hizo za Mashamba kuwakodisha wakazi hao kwa gharama halikadhalika kuutumia mfereji wa mradi wa kijiji hicho kwa maslahi yake binafsi.



Post a Comment

Theme images by Maliketh. Powered by Blogger.